MONUSCO yapatiwa mamlaka mpya ili kuimarisha amani DRC

Kusikiliza /

Nembo ya MONUSCO

Hatimaye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2098 ambalo pamoja na mambo mengine linapatia ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ay Kongo, DRC, MONUSCO mamlaka mpya kwa ajili ya kuwezesha kupatikana amani ya kudumu nchini humo.

 Msimamizi Mkuu wa masuala ya ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema kwa mujibu wa azimio hilo, MONUSCO sasa inaweza kupeleka yenyewe brigedi ya kuingilia kati mashambulizi au kushirikiana na serikali ya DRC kwa lengo la kupunguza uwezo wa vikundi vyenye silaha na vitisho kwa mamlaka za nchi na usalama wa raia.

(Sauti ya Herve Ladsous)

Ladsous amesema hatua hiyo ni ya kipekee na muhimu katika kung'oa mzizi wa mgogoro na kumaliza madhila yanayokumba raia wa DRC.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Raymond Tshibanda N’tungamulongo ambaye ameshuhudia kupitishwa kwa azimio amewaambia waandishi wa habari kuwa kama serikali wameridhishwa na wana matumaini makubwa.

 ( Sauti ya N'tungamulongo)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031