Mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake yatiwa shime

Kusikiliza /

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, amesema mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake hayahitaji mpambanajii awe mwanasiasa wala mtunga sera.

Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume inayohusika na maswala ya Wanawake katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kila mtu kwa nafasi yake anaweza kupambana na ukatili dhidi ya wanawake akitolea mfano wa mchezaji wa mpira nchini Cameroon aliyetumia taaluma yake kufikisha ujumbe wa mapambano hayo kwa kusema kuwa mshindi pambana na ukatili dhidi ya wanawake.

Bwana Jan amesema ni wakati kwa wanaume na wavulana kuchukua nafasi katika mapambano hayo ili kutimiza lengo.

(SAUTI YA JAN)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031