Haki ya kufanya kazi ni ya wote: Pillay

Kusikiliza /

 

Watu wenye ulemavu wakiwa kazini

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa haki ya kufanya kazi ni haki iliyo muhimu lakini mamilioni ya watu walio na ulemavu kote duniani wanaendelea kunyimwa haki hiyo na pia kunyimwa fursa ya kushiriki kwenye ujenzi wa jamii zao.

Pillay amesema kuwa kuna changamoto tatu ambazo mara nyingi huwakumba watu wenye ulemavu zikiwemo ugumu wa kuyafikia maeneo ya kazi moja kwa moja , Kushindwa kupata elimu inayohitajika na mafunzo kwenye nyanja mbali mbali mbali kutokana na kasumba kuwa hawatapata ajira kwenye sekta wazi zilizoko na pia kutoshirikishwa kwa watu walemavu kwenye masuala yanayohusu sera mafunzo na ajiara.

(SAUTI YA PILLAY)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031