Majeshi ya Burundi yakomboa wananchi kwa kutoa tiba nchini Somali

Kusikiliza /

Wiki hii Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalai (AMISOM) ambao umekasimiwa mamlaka na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatimiza maadhimisho ya sita tangu uwasili nchini Somalia huku ukikabiliwa na changamoto mbalimbali lakini pia maadhimisho hayo yakitaja baadhi ya mafanikio kama vile kuimarika kwa usalama na huduma za afya.

Licha ya usalama kuimarika nchini Somalia wengi wa wakimbizi walioko katika kambai mbalimbali hawapati huduma bora kama vile malazi bora ambapo wanatumia mifuko ya plastiki kujifunika huku wakipokezana vitanda.

Majeshi ya Burundi chini ya majeshi ya umoja wa Afrika nchini Somalia yaliyoko nchini humo tangu mwaka 2007 wakati mapigano mitani,mauaji na milipuko yalipochukua kasi yamekuwa yakifanya kazi kubwa ya kutibu kwa  wagonjwa ambao hawahitaji kulazwa.Kazi hii hufanywa  chini ya Majeshi ya Somali na Ujumbe wa Afrika Somali katikamaeneo ya chuo kikuu cha taifa cha zamani.

Majeshi  hayo yamekuwa yakitoa huduma kitabibu bure mara mbili kwa wiki na wakati mwingine chakula kwa wakimbizi wa ndani na watu wengine katika jamii.

Sekta ya afya nchini Somali ilizorota vita ilipoanza nchini humo baada ya kuangushwa kwa utawala wa Said Bare mwaka 1991.

Mana Muhamed  ni mmooja wa wakazi ambaye amewahi kiutibiwa katika vituo hivyo na anasema

SAUTI (MANA MUHAMEDI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930