Licha ya maendeleo ya kisiasa janga la misaada ya kibinadamu ni tishio Yemen

Kusikiliza /

Kundi la Misaada ya Kibinadamu nchini Yemen limehadharisha kwamba ikiwa hatua za dharura juu ya misaada ya kibinadamu hazitachukuliwa nchini humo, hakutakuwa na hatua za kimaendeleo.

Hadhari hiyo inatolewa wakati ambapo marafiki wa Yemen wanakutana mjini London, Uingereza kujadili hali ya kisiasa, kiuchumi na usalama wa nchi hiyo iliyoko kwenye kipindi cha mpito.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ambaye pia ni Mratibu shughuli za misaada ya kibinadamu Ismail Ahmed amesisistiza kuwa licha ya kuwepo kwa maendeleo ya kisiasa, tatizo la misaada ya kibinadamu bado lipo na amelitaka kundi la marafiki wa Yemen na wahisani wengine kuchangia mpango wa misaada ya kibinadamu wa Yemen wa mwaka 2013

Mpango huo unahitaji dola Milioni Mia Saba Kumi na Sita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031