Kuimarika kwa usalama Somalia, wavuvi wajikwamua

Kusikiliza /

Bandari ya Mogadishu

Kufuatia kuimarika kwa hali ya usalama nchini Somalia baada ya majeshi ya Kikosi cha muungano wa Umoja wa Afrika AMISOM kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya nchi hiyo kukiondoa kikundi cha kigaidi cha Alshabaab mjini Mogadishu, wakazi wa mji huo sasa wanaendelea na shughuli za kukuza kipato ikiwemo kushiriki shughuli za uvuvi. Mmoja wa wavuvi wa samaki katika mji huo Ahmed Akar anajivunia kuimarika kwa usalama ambako amesema kunampatia fursa ya kufanya kazi hiyo.

SAUTI ( AHMED EKAR)

 ” Wakati mwingine  tunapata samaki wengin ila wakati mwingine tunapata kidogo, kama samaki ni mdogo tunapata  dola 12 kwa kilo, hii ni kwa samaki aina ya nguru. Tukipata kidogo ni dola Sita kwa kilo. Kwa sasa aina hii ya samaki ni chache na wanahitajika sana.”

Kwa upande wake waziri mpya wa rasilimali nchini Somalia  Abdirizak Mohamed, anasema ulinzi zaidi unahitajika baharini ili kukomesha mambo mengi yanayofanyika kinyume cha sheria ambayo huzuia shughuil za kukuza kipato kupitia sekta ya uvuvi nchini humo.

SAUTI  (WAZIRI ABDILIRIZAK)

” Hatuna walinzi wa baharini, kwa sababu hiyo kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria kwenye bahari yetu. Hatuna uwezo wa kufanya kitu kwa sasa lakini hilo litashughulikiwa kwa mujibu wa sera za serikali."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031