Kongamano la UM kujadili mauzo ya nje ya nchi zinazoendelea

Kusikiliza /

Mashirika matano ya Umoja wa Mataifa yameandaa kongamano la siku mbili kuhusu mauzo ya nje ya bidhaa kutoka nchi zinazoendelea. Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo, ni pamoja na chagamoto zinazozikumba nchi zinazoendelea, zikiwemo kuainisha bidhaa za kahawa, chai, kakao, ndizi, samaki, mbao na maua kama bidhaa endelevu chini ya mipango tofauti ya kutoa vibali

Mashirika husika ni lile la Chakula na Kilimo ( FAO), Kamati ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Lile la Mazingira (UNEP), lile la Viwanda na Maendeleo (UNIDO) na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC).

Kongamano hilo la Machi 21 hadi 22 ni sehemu ya juhudi za mashirika ya Umoja wa Mataifa za kuwa na njia taratibu ya vyombo muhimu vya kupima biashara endelevu na maendeleo endelevu na litajadili viwango vya uendelevu vinavyoathiri mauzo ya nje kutoka nchi zinazoendelea.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031