IOM yataka wahamiaji wajumuishwe kwenye tiba ya TB

Kusikiliza /

Kampeni ya kutokomeza Kifua Kikuu

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya Kifua Kikuu tarehe 24 mwezi huu, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limataka kujumuishwa kwa wahamiaji kwenye mikakati  ya kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu. Hii ni baada ya ripoti zinazosema kuwa ugonjwa wa kifua kikuu umesalia kuwa mzigo mkubwa  sehemu nyingi za ulimwengu ukiwaathiri zaidi  watu maskini na wale wanaobagulia hususan wahamiaji. Mkurugenzi Mkuu wa IOM William Lacy Swing amesema mara nyingi progamu za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu zinawaengua wahamiaji na IOM imeripoti kucheleweshwa kwa tiba au kutotolewa kabisa kwa tiba dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu.  Amesema tafiti nyingi zinaonyesha kuwa vyanzo vya vifo vingi vya wahamiaji na familia zao ni magonjwa yahusianayo na Kifua  Kikuu lwa kuwa mara nyingi hawawezi kufanya uchunguzi wa afya dhidi ya ugonjwa huo au ukupata tiba endelevu.

 

Hata hivyo amesema kwa ushirikiano na shirika la afya duniani, WHO, kwa sasa IOM inatekeleza mpango wa kupambana na kifua kikuu miongoni mwa wahamiaji huko Thailand, Nepal, Cambodia, Ethiopia, Ghana na Myanmar.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031