IOM na washirika wazuru Sudan,wabaini hali tete za afya kwa maelfu ya raia.

Kusikiliza /

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi na misaaada ya kibinadamau kwa kushirikiana na mwakilishi wa serikali ya Uingereza wamefanya ziara katika maeneo ya wazi katika mji mkuu wa Sudan Khartoum ambako maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakipokezana malazi wakati wanasubiri kurejea nyumbani.

 Mashirika hayo yanaoyoongozwa na Shirika la Umoja wa Mataifaifa la Uhamiaji, IOM, UNOCHA na UNHCR yametembelea maeneo mawili kati ya arobaini yanayotawaliwa na raia wa Sudan Kusini wanaokadiriwa kuwa elfu arobaini na kubaini kuwa watu hao wanaishi katika mazingira hatarishi,wakiwa hawana chakula cha kutosha,maji na huduma za afya zikiwa zimezorota.

 Raia hao wanaishi katika nyumba zisizo salama zilizojengwa kwa malighafi laini inayohatarisha maisha yao hususani wakati wa mvua.Pia Kukosekana kwa huduma za afya na huduma stahiki za vyoo kwa raia hao wa Sudan Kusini kumetajwa kama sababu mojawapo ya kuhatarisha  maisha yao husuani wakati wa mafuriko.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31