Idadi ya wakimbizi wa Syria Uturuki yaongezeka: Guterres atembelea kambi

Kusikiliza /

Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres akiwa katika kambi moja huko Uturuki

Idadi ya raia wa Syria walio wakimbizi nchini Uturuki kwa sasa imefikia zaidi ya Laki Mbili na Nusu baada ya serikali kuanza kuwaandikisha pamoja na wale walio nje ya kambi 17 zinazosimamiwa na serikali. Taarifa hiyo zinajiri huku mkuu wa Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres akiwa ziarani nchi jirani na Syria. Tayari ametembelea kambi za Uturuki na anatarajiwa kuitembelea kambi ya Za'atri nchini Jordan  na kituo cha usajili cha Irbib kabla ya kulekea nchini Lebanon. UNHCR inasema kuwa uandikishaji wa wakimbizi na usimamizi wa kambi vinaendeshwa na shirika la AFAD kwa ushirikiano na Shirika la msalaba mwekundu nchini Uturuki. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA Adrian)

Jambo muhimu la hivi punde ni kwamba Uturuki imeanza kuwaandikisha wakimbizi wa Syria walio nje ya kambi za wakimbizi na sehemu za mijini. Awali ilikuwa imejumulisha kwenye orodha zake wakimbizi wale wanaoishi kwenye kambi 17 waliko wakimbizi 186.000. Wakimbizi 40,000 walio mijini wamendikishwa hadi sasa kuambatana  na sera mpya huku wengine 30,000 zaidi wakisubiri kuandikishwa. Tatizo lililopo ni kwamba idadi ya wakimbzi walioandikishwa nchini Uturuki inazidi kupamba na sasa inasimamia watu 258,200.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031