Idadi ya wakimbizi wa Kipalestina yaongezeka Syria.

Kusikiliza /

nembo ya UNRWA

Mapigano yanayoendelea nchini Syria yameendelea kusababisha vifo na idadi ya wakimbizi, na misaada zaidi ya kibinadamu inahitajika.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, idadi ya wakimbizi wa kipalestina walioko Syria wanaohitaji misaada ya kibinadamu imeongezeka na kufikia laki nne, huku wakimbizi wa Palestina waliokimbilia Jordan wakifikia zaidi ya elfu nne, na huko Lebanon,  wakimbizi zaidi ya elfu 30.

Kwa sasa kuna wakimbizi wa Kipalestina zaidi ya elfu 11 wa ndani nchini Syria ambapo kati ya hao, takribani elfu nane wanahifadhiwa katika majengo ya  UNRWA, kama vile shule na vituo vya mafunzo vinavyotumika kama malazi ya muda. Mpaigano yanatajwa kukuwa zaidi  katika maeneo ya Damascus, Allepo, Dera na Homs.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930