Hatua zichukuliwe kutokomeza dhuluma dhidi ya wanawake: UN Women

Kusikiliza /

Katika ujumbe wake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Kitengo cha Wanawake katika Umoja wa Mataifa, (UN WOMEN) Michelle Bachelet, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutimiza ahadi zake na kulinda haki ya wanawake kuishi bila kudhulumiwa.

Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu inakuja wakati mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake, ambao unaangazia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Bi Bachelet amesema ingawa kuna changamoto kubwa kukabiliana na ukatili huu unaoathiri wanawake saba kati ya kila kumi kote duniani, inawezekana kuwa na mabadiliko, kwani sasa tayari mabadiliko yanatekelezwa katika maeneo mengi duniani. Ametoa wito kwa serikali ziongeze kasi ya kutekeleza sera zenye malengo ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930