Guterres asifu Albania kupokea wakimbizi wa Iraq

Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi, UNHCr, António Guterres, amesema kitendo cha serikali ya Albania kukubali kuwapokea wakimbizi wa Iraq waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi ya Hurriya ni hatua ya kutia matumaini na ameipongeza na kuikaribisha.  Albania imekubali kuwapokea wakimbizi hao 210 walikuwa wamehifadhi kwa muda katika kambi ya Hurriya ambayo pia hujulikana kama kambi ya ukombozi. Kambi hiyo pia inakabiliwa na raia wanakadiriwa kufikia 3000.  Bwana Guterres amesema kuwa kitendo kilichoonyeshwa na Albania ni uungwana wa hali ya juu na kionaonyesha jinsi dunia inavyopaswa kushirikiana kuzikabili changamoto mbalimbali.  Katika siku za hivi karibuni hali ya usalama katika eneo hilo la kambi ilikuwa tete kutokana na matukio ya mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na wakazi wa eneo hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930