Cote D'Ivoire yatakiwa iendeleze demokrasia kwa kulinda haki za binadamu na sheria

Kusikiliza /

Doudou Diene

Mtaalam huru kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cote d'Ivoire, Doudou Diene, amesema kuwa nguzo tatu za mzozo wa nchi hiyo, ambazo athari  za kimaadili, kisiasa na kijamii, zinatakiwa kuzingatiwa kwa njia ya kina.

Akiongea kwenye kikao cha 22 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea mjini Geneva, Uswisi, Bwana Diene amesema uhasama wa kisiasa umeendelea kuwa changamoto kubwa, licha ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea. Ameongeza kuwa changamoto nyingine kuu ni watu kutowajibika kwa uhalifu na suala la usawa katika mfumo wa sheria.

Mtaalam huyo huru amependekeza kuwa mfumo wa sheria unatakiwa usiwe na upendeleo, na ukiukaji wa haki za binadamu ukabiliwe kisheria

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031