Burundi yajiandaa kwa uchaguzi mkuu, Ban atoa ujumbe

Kusikiliza /

Wachuuzi katika soko kuu mjini Bujumbura, Burundi

Nchini Burundi, harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zimeanza na tayari ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi, BNUB imeitisha kikao cha wanasiasa nchini humo kinachonuwia kumaliza uhasama na kuandaa  vema uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015.

Kikao hicho kinawakutanisha wanasiasa wa chama tawala pamoja na wale wa upinzani ambao baadhi yao wamerejea nchini  wiki iliyopita na kubwa zaidi ni kujadili dosari zilizojitokeza katika  uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuangazia vema uchaguzi wa mwaka wa 2015. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametolea mwito  wanasiasa  hao  kuwa wazi kwenye mazungumzo yanayojenga ili kuchora mustakbali mzuri wa taifa la Burundi.

Je ni yapi yamejiri huko mwandishi wetu wa Maziwa Makuu, Ramadhan Kibuga na maelezo zaidi.

 (SAUTI Ramadhani)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031