Baraza la Usalama lalaani shambulizi la bomu kwenye msikiti Syria

Vitaly Churkin, Balozi wa Urusi UM

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulizi la kigaidi kwenye msikiti mjini Damascus, Syria, ambalo lilifanyika mnamo Machi 21, na kuwaua zaidi ya watu 40, kumjeruhi kiongozi wa kidini na kuwajeruhi watu wengine kadhaa.

Katika taarifa ilotolewa na Rais wa Baraza hilo kwa mwezi Machi, Balozi Vitaly Churkin wa Urusi, wanachama wa Baraza hilo wamerejelea azma yao ya kulaani vitendo vyote vya ghasia vinavyoelekezwa kwa raia.

Wamesema ugaidi wa aina zote ni mojawapo ya tishio kubwa zaidi kwa amani ya kimataifa na usalama, na vitendo vyovyote vya kigaidi ni vya kihalifu na havikubaliki, bila kuzingatia kinachovichochea, wapi vinapofanyika na nani anayevifanya.

Wameelezea kusikitishwa kwao na kutuma risala ya rambi rambi kwa jamaa wa wahanga wa shambulizi hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2015
T N T K J M P
« nov    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031