Baraza la Haki za Binadamu lajadili maeneo ya Wapalestina yalokaliwa

Kusikiliza /

Bi Chritine Chanet

Baraza la Haki za Binadamu leo limefanya mazungumzo na tume ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu jinsi haki za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni za Wapalestina katika maeneo yalokaliwa na Waisraeli zinavyoathiriwa, ikiwemo mashariki ya Jerusalem.

Mkuu wa tume hiyo, Christine Chanet amesema kuendeleza kazi ya ujenzi kwenye maeneo hayo ni njia moja ya ukoloni ambayo inadunisha haki ya kujitawala ya watu wanaoishi katika maeneo hayo yalokaliwa.

Ameongeza Israel inatakiwa ikomeshe mara moja hizi harakati za kikoloni, ianze kuondoa ulowezi uliopo sasa na kuhakikisha utulivu umerejea.

(SAUTI YA CHRISTINE CHANET)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930