Ban amteua Meja Jenerali Edson Leal Pujol kuwa kamanda wa kikosi cha MINUSTAH nchini Haiti

Kusikiliza /

MINUSTAH katika ziara ya ulinzi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amemteua Luteni Jenerali Edson Pujol kutoka Brazil kuwa kamanda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Haiti (MINUSTAH) .

Luteni Pujol anachukua mahala pa Meja Jenerali Fernando Rodriguez Goulat ambaye pia ni raia wa Brazil ambaye alikamilisha majumu yake kama kamanda wa MINUSTAH tarehe 27 mwezi huu.

Bwana Ban ameisifu kazi aliyoifanya Meja Rodriguez kama kamanda wa MINUSTAH akisema kuwa ujuzi wake na pia kujitolea vilichangia pakubwa kwenye jitihada za Umoja wa Mataiafa za keleta utulivu nchini Haiti. Luteni Jenerali Pujol ana ujuzi mwingi kuhudumu katika wadhifa huo.

Alijiunga na jeshi la Brazil mnamo mwaka 1971 na ameshahudumu kwenye nyadhifa za juu kwenye jeshi la Brazil. Mnamo mwaka 2009 aliteuliwa kama kamanda wa taasisi ya mafuzno ya kijeshi.

Hadi kuteuliwa kwake Meja Pujol alikuwa akihudumu kama mkuu wa kituo cha ujasusi wa kijeshi. Alizaliwa mwaka 1955 na ana mke na watoto wawili.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031