Ban amsifu Bachelet wakati akiondoka UN WOMEN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemsifu Bi Michelle Bachelet kwa kazi yake ilofa wakati akihudumu kwenye wadhfa wa Mkuu wa kitengo cha Wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women.

Bi Bachelet ametangaza nia yake kujiuzulu kutoka wadhafa huo mara tu baada ya kumalizika mkutano kuhusu hadhi ya wanawake, ambao umekamilika mjini New York mnamo siku ya Ijumaa, Machi 15.

Katika taarifa yake, Bwana Ban amemsifu Bi Bachelet kama mtu aliyefaa kushikilia wadhfa wake, hususan kama kiongozi wa kitengo hicho tangu kilipozinduliwa mnamo Julai mwaka 2010.

Amesema ufanisi wake ni pamoja na kuweka mikakati mipya ya kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya ukatili, na kuendeleza uelewa kuwa kuwapa uwezo wanawake ni lazima kuwe sehemu muhimu ya kazi ya Umoja wa Mataifa. Bwana Ban amesema ataendeleza juhudi hizo, kwa kutumia msingi aliouweka Bi Bachelet.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031