Ban ameteua mkuu wa ujumbe wa kuhakiki madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria

Kusikiliza /
Msemaji wa Katibu Mkuu

Martin Nesirky

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Profesa Ake Sellström kutoka Sweden kusimamia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuhakiki ripoti za madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Martin Nesirky.

Bwana Sellström ni meneja wa miradi katika taasisi ya utafiti nchini Sweden, ambayo ni kituo cha masomo ya juu kuhusu jamii, usalama na hali za hatari, na hususan matukio makubwa yanayohusisha vitu vya kemikali, bayolojia, na miyale ya nyuklia na vilipuzi.

Bwana Sellström pia ni mwanasayansi maarufu, na mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya kusalimisha silaha na usalama wa kimataifa. Amefundisha katika vyuo vikuu Marekani, na kuwahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa kiejeshi na usalama nchini Sweden.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031