Ban afanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame mjini New York

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais Paul Kagame wa Rwanda

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mjini New York ambapo walizungumzia hali iliyopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo  DRC  kufuatia kutiwa sahihi kwa makubaliano ya amani na usalama kama chombo ya ufumbuzi kwa chanzo cha mizozo katika eneo la maziwa makuu.

Wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwa karibu na mjumbe wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Mary Robinson katika jitihada za kuunga mkono  utekelezwaji wa makubaliano hayo.

Ban alieleza umuhimu kwa mataifa yote eneo hilo kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC na kukaribisha kujisalimisha kwa mbabe wa kivita Bosco Ntaganda kwa ubalozi wa  Marekani mjini Kigali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930