Balozi Mahiga alaani shambulio la mjini Mogadishu

Kusikiliza /

Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ameeleza kushtushwa na kusikitishwa kwake na shambulio la bomu  lililotokea kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu. Tukio hilo limetokea baada ya gari lililokuwa na vilipukaji kulipuka ambapo taarifa za awali zinadokeza kuwa takribani watu Saba wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Taarifa nyingine zinadokeza huenda afisa usalama wa Somalia alikuwa mlengwa wa shambulio hilo. Balozi Mahiga pamoja na kutuma rambirambi kwa familia na pole kwa majeruhi amesema shambulio hilo la leo halikubaliki kabisa. Amesema Somalia imekuwa ikisonga mbele katika kuendeleza amani na utulivu na hivyo shambulio hilo la kigaidi kitazidi litaongeza ari ya wasomalia ya kuendeleza jitihada za amani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031