Askari wa UNDOF waachiwa huru, Ban apongeza

Kusikiliza /

Kikosi cha UNDOF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amepongeza hatua ya kuachiwa huru na wakiwa salama walinzi wa amani 21 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo kwenye maeneo huru ya uangalizi, UNDOF waliokuwa wanashikiliwa tangu tarehe Sita mwezi huu kwenye eneo la Al Jamla huko Mashariki ya Kati.

Taarifa ya Bwana Ban iliyotolewa na msemaji wake imemkariri akishukuru jitihada zote zilizowezesha kuachiwa huru kwa walinzi hao wa amani walio katika eneo huru kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano kati ya Syria na Israel.

Katibu Mkuu amesisitiza kwa pande zote husika kuwa walinzi hao wa amani wa Umoja wa Mataifa hawaegemei upande wowote na kuzitaka pande hizo kuheshimu uhuru wa askari wa UNDOF kutembea bila vikwazo vyoyote katika mazingira salama huku akitaka pande hizo kuheshimu na kutambua haki za raia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930