Askari 10 wa M23 wajisalimisha kwa MONUSCO, idadi sasa ni zaidi ya 90

Kusikiliza /

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUSCO umetangaza kujisalimisha kwa askari 10 wa kikundi cha waasi cha M23. Taarifa ya MONUSCO imesema kuwa askari hao wanane ni maafisa polisi wa DRC na wawili ni askari wa Rwanda na walijisalimisha mwezi uliopita kwenye ofisi za ujumbe huo huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini. Askari hao wametaja sababu za kujisalimisha kuwa ni ubaguzi ndani ya kikundi hicho cha waasi hususan kwenye masuala ya mishahara na kupandishwa vyeo. Tayari wamekaguliwa na utambulisho wao kuthibitishwa na wamesema idadi kubwa ya wenzao wangalipenda kukihama kikundi hicho. Kwa mujibu wa MONUSCO askari wa Rwanda watarejeshwa kwao kwa mujibu wa taratibu. Zaidi ya askari 90 wa M23 wameripotiwa kujisalimisha MONUSCO tangu tarehe Mosi mwezi Disemba mwaka jana.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29