Nyumbani » 28/03/2013 Entries posted on “Machi 28th, 2013”

Ban asifu MONUSCO kupatiwa mamlaka mpya

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono hatua aliyoitaja kuwa ni muhimu ya Baraza la Usalama kupitisha azimio juu ya Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo, DRC ambalo linaipatia ujumbe wa Umoja huo nchini humo MONUSCO mamlaka mpya. Katika taarifa yake Ban amesema azimio hilo ni hatua madhubuti ya kushughulikia chanzo cha mgogoro [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yapatiwa mamlaka mpya ili kuimarisha amani DRC

Kusikiliza / Nembo ya MONUSCO

Hatimaye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2098 ambalo pamoja na mambo mengine linapatia ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ay Kongo, DRC, MONUSCO mamlaka mpya kwa ajili ya kuwezesha kupatikana amani ya kudumu nchini humo.  Msimamizi Mkuu wa masuala ya ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makambi ya wakimbizi wa ndani yalindwe zaidi:UM

Kusikiliza / Kambi

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kulinda makambi ya wakimbizi wa ndani kufuatia shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Pakistan. Mtaalamu Chaloka Beyani ambaye ni mwakilishi maalumu wa haki za binadamu kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani amelaani vikali tukio hilo la Machi 21 kwenye [...]

28/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNDP kukwamua wajasiriamali

Kusikiliza / Mfano wa biahsara ya kutuma pesa, Zambia

Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP  kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo umeanzisha mpango utakawawezesha wajasiriamali na sekta binafsi kwa ujumla kukuza kipato  kwa haraka na kwa njia rahisi. Mpango huo unaofahamika kama wito wa hatua za kibiashara ni mahususi kwa ajili ya kupambana na umaskini na  unalenga zaidi kukuza vipato vya wajasiriamali [...]

28/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF wawaandalia watoto wakimbizi mazingira rafiki

Kusikiliza / Wakimbizi wa kutoka DRC

Zaidi ya wakimbizi elfu 68 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia Rwanda kutafuta makazi kufuatia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo,  iliyotawaliwa na vita kwa miongo kadhaa. Utengano wa kifamilia imekuwa ni moja ya kadhia kubwa wanyokutana nayo wakimbizi ambao mara nyingi husambaratika wakati wa kukimbia mapigano. Waathirika wakubwa katika hili ni watoto ambao [...]

28/03/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Taifa la Mongolia latakiwa kutumia fursa zilizopo kuinua uwekezaji

Kusikiliza / Bendera ya Mongolia

Tathmini kuhusu uwekezaji kutoka kwa shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD inayopendekeza kuwa taifa la Mongolia linastahili kutumia fursa ilizopota miaka ya hivi karibuni ya uwekezaji wa kimataifa kwenye sekta ya uchimbaji wa madini itajadiliwa na waziri mkuu wa nchi hiyo na mafisa wengine wa ngazi za juu serikalini. Kwenye mkutano [...]

28/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasaidia watoto wakimbizi Rwanda

Kusikiliza / Mkimbizi wa DRC kambini Rwanda

Kufuatia maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kukimbia na kutafuta hifadhi katika nchi mbalimbali ikiwamo Rwanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto UNICEF, na washirika linahudumia watoto walioko katika kambi hizo ili kuwaandalia mazingira rafiki. Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNICEF nchini Rwanda Noala Skinner, idadi ya watoto katika [...]

28/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Indonesia yatakiwa kusitisha hukumu ya kifo

Kusikiliza / Christof Heyns

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu hukumu ya kifo Christof Heyns Alhamisi ameitaka serikali yaIndonesia kudhibiti utekelezaji wa hukumu ya kifo katika kutekeleza wajibu wake wa kimataifa. Tamko hilo limekuja baada ya  taarifa kwamba nchi hiyo imetekeleza hukumu ya kwanza ya kifo dhidi ya bwana Adanmi Wilson tangu Novemba 2008 licha ya ombi la [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa kibinadamu waongezeka CAR: OCHA

Kusikiliza / OCHA inasema mgogoro waongezeka CAR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema mgogoro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwemo kutwaliwa madaraka kwa nguvu kulikofanywa na kundi la Seleka Machi 24 kumechangia hali ya kibainadamu ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya zaidi. Tangu Desemba mwaka jana inakadiriwa kuwa watu 173,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani huku [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Meja Jenerali Edson Leal Pujol kuwa kamanda wa kikosi cha MINUSTAH nchini Haiti

Kusikiliza / MINUSTAH katika ziara ya ulinzi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amemteua Luteni Jenerali Edson Pujol kutoka Brazil kuwa kamanda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Haiti (MINUSTAH) . Luteni Pujol anachukua mahala pa Meja Jenerali Fernando Rodriguez Goulat ambaye pia ni raia wa Brazil ambaye alikamilisha majumu yake kama kamanda wa MINUSTAH [...]

28/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vijana wakutana UM kujadili teknolojia katika maendeleo endelevu

Kusikiliza / Vijana kwenye kongamano New York

Ni vipi vijana wanaweza kushiriki kuziba pengo la kidijitali na kuchangia juhudi za kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu, yaani SDGs? Hilo ndilo lililokuwa swali vichwani mwa mamia ya vijana kutoka kote duniani, wakati wa kongamano ambalo limehitimishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Jumatano jioni. Kongamano hilo liliwaleta pamoja vijana wanaojihusisha [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia, Mawasiliano mbalimbali, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama kupitisha azimio kuhusu DRC

Kusikiliza / Baraza la Usalama kuangalia upya MONUSCO

Baraza la Usalama baadaye leo linatarajiwa kupiga kura juu ya rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Ufaransa kuhusu shughuli za ulinzi wa amani huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo. Mapendekezo hayo yanazingatia ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC na nchi za Maziwa Makuu ambayo pamoja na mambo mengine imependekeza kuangaliwa upya kwa [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali inazidi kuzorota Syria: UNHCR

Kusikiliza / Hali inaendelea kuzorota Syria

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema hali inaendelea kuzorota nchini Syria ikiwemo katika maeneo ya Kati na viunga vya Damascus na hivyo kusababisha ongezeko la wakimbizi. Shirika hilo linasema sasa kuna hofu ya usalama wa kikanda wakati idadi ya wakimbizi waliohama nhi hiyo nakwenda Misri, Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki ikifikia [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama latilia shaka usalama wa Milima ya Golan

Kusikiliza / Usalama katika milima ya Golan

Baraza la Usalama limetaka pande zinazozozana nchini Syria kutohatarisha usalama wa watumishi wa Umoja wa Mataifa walioko katika milima ya Golani. Katika taarifa yake, Baraza hilo limeelezea masikitiko yake kutokana na kuzidi kuongezeka kiwango cha askari katika eneo hilo ambalo wako watumishi wa Umoja wa Mataifa walioko kwenye kikosi maalumu cha ufuatiliaji zoezi la kuondoa [...]

28/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatma kuhusu askari wa kulinda amani wa UM nchini Mali wiki ijayo

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo litakuwa na kikao maalum kuhusu Mali ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe watajadili uwezekano wa kupeleka kikosi cha kuweka utulivu nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mashauriano ya faragha ya wajumbe wa baraza hilo, Mwakilishi Maalum wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Balozi [...]

28/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031