Nyumbani » 25/03/2013 Entries posted on “Machi 25th, 2013”

Amani yakwamua shughuli za uvuvi Somalia

Kusikiliza / uvuvi Somalia

Somalia!  Nchi ambayo imekuwa katika mapigano kwa muda mrefu jambo lililosababisha  kuharibika kwa miundombinu na uchumi wa nchi kuporomoka . Nchi hiyo ambayo imeanza kuimarika kiusalama iko katika mchakato wa ujenzi wa uchumi katika sekta mbalimbali  ikiwamo ya uvuvi. Somalia inajivunia  rasilimali kama vile ukanda wa Pwani ulio mrefu kuliko yote barani Afrika wenye kilometer [...]

25/03/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa FAO asifu mwenendo wa uzalishaji chakula mdogomdogo vijijini

Kusikiliza / zao la mhogo

Wakulima wadogowadogo, uzalishaji na ununuzi wa nyumbani pamoja na kuibua tena ukuzaji wa mimea ya kijadi kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza njaa, amesema leo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, wakati akiwahutubia wahadhiri na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Chakula nchini Italia. Bwana da Silva ameelezea kuwepo kwa uwezekano [...]

25/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maonyesho ya mwaka 2015 kuhusu chakula kuandaliwa nchini Italia

Kusikiliza / expo2015

Suala la kuhakikisha kuwepo kwa mifumo salama ya chakula litakuwa ajenda kuu kwenye maonyesho ya mwaka 2015 mjini Milan nchini Italia, kwa mujibu wa naibu Mkurugenzi mkuu wa kitengo cha misitu kwenye Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa  FAO Eduardo Rojas-Briales. Kauli mbiu ya maonyesho hayo itakuwa "Kuilisha Sayari, Nguvu kwa Maisha". [...]

25/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Kipalestina yaongezeka Syria.

Kusikiliza / nembo ya UNRWA

Mapigano yanayoendelea nchini Syria yameendelea kusababisha vifo na idadi ya wakimbizi, na misaada zaidi ya kibinadamu inahitajika. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, idadi ya wakimbizi wa kipalestina walioko Syria wanaohitaji misaada ya kibinadamu imeongezeka na kufikia laki nne, huku wakimbizi wa Palestina waliokimbilia Jordan wakifikia zaidi [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kundi la BRICS lazidi kushamiri kwenye uwekezaji wa nje

Kusikiliza / brics

Ripoti mpya ya chombo cha kufuatilia mwelekeo wa uwekezaji duniani, GITM imedhihirisha ongezeko la vitegauchumi vya kigeni duniani hususan barani Afrika kutoka kundi la nchi za BRICS ambazo ni Brazil, Urusi, Afrika Kusini, China na India. Ripoti hiyo iliyotolewa leo siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi wakuu wa BRICS huko Durban Afrika [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili harakati za amani Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu maalumu wa UM kuhusu Mashariki ya Kati, Robert Serry, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika ripoti yake kuwa hali ya mvutano baina ya Israeli na Palestina bado imesalia kuwepo, licha ya kwamba vitendo ambavyo vinaleta kutokuaminiana vimepungua.  Amesema mathalan katika kipindi ambacho ripoti hiyo ilikuwa inaandaliwa, hakukuwepo na tangazo la ujenzi [...]

25/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahiga alaani mauaji ya mwandishi wa habari mjini Mogadishu

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Augustine Mahiga, ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji ya mwandishi wa habari, Rahma Abdulkadir aliyekuwa akifanya kazi na Redio ya Abduwaq. Watu wasiojulikana wanaripotiwa kumshambulia Bi Abdulkadir kwa bastola na kumuua katika mtaa wa Yaqshid, mjini Mogadishu. Bwana Mahiga amekilaani vikali kitendo hicho, akisema kuwa Somalia inaendelea [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi za UM Bangui zaporwa: OCHA

Kusikiliza / Mkazi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kutokana na hali ya usalama kuwa tete huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa umesema utawaondoa wafanyakazi wake wasiohitajika kutoka  mji mkuu Bangui baada ya waasi kutwaa mamlaka ya nchi hiyo.  Watakaohamishwa watapelekwa kwenye makao ya muda mjini Yaounde nchini Cameroon. Ofisi za mashirika kadha ya Umoja wa Mataifa zimeporwa na vifaa kuharibiwa [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuimarika kwa usalama Somalia, wavuvi wajikwamua

Kusikiliza / Bandari ya Mogadishu

Kufuatia kuimarika kwa hali ya usalama nchini Somalia baada ya majeshi ya Kikosi cha muungano wa Umoja wa Afrika AMISOM kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya nchi hiyo kukiondoa kikundi cha kigaidi cha Alshabaab mjini Mogadishu, wakazi wa mji huo sasa wanaendelea na shughuli za kukuza kipato ikiwemo kushiriki shughuli za uvuvi. Mmoja wa [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wawakumbuka waathiriwa wa utumwa

Kusikiliza / Minyororo ya utumwa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo linafanya hafla maalum ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa iliyofanyika kupitia Bahari ya Atlantiki. Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kauli mbiu 'Daima huru: kusherehekea ukombozi', kama kumbukumbu ya ukombozi wa watumwa kote duniani. Siku hii inaadhimishwa kwa heshima ya [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNWRA yalaani mauaji ya watoto wa Kipalestina nchini Syria

Kusikiliza / Mtoto wa kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uratibu wa misaada ya usamaria mwema kwa wakimbizi wa Kipalestina UNWRA, limelaani vikali tukio la mauaji ya wakimbizi watoto watano wa kipalestina nchini Syria na kuonya uwezekano wa mzozo huo kuvuruga ustawi wa vijana.  Kulingana na taarifa za UNWRA,kuuawa kwa watoto hao kunazidisha hali ya wasiwasi juu ya [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani kile alichokiita kuchukua madaraka kwa njia isiyo ya kikatiba kulikofanywa na waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.  Bwana Ban amesema amesikitishwa na taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu, na kusisitiza juu ya kuheshimiwa kwa makubaliano ya amani ya Libreville ambayo amesema kuwa ndiyo yatayotoa [...]

25/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031