Nyumbani » 22/03/2013
Entries posted on “Machi 22nd, 2013”
Kusikiliza /

Machi 24 kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya ugonjwa wa kifua kikuu. Makala yetu wikii hii inajikita katika maadhimisho hayo yatakayofanyika mwishoni mwa juma. Ugunduzi rasmi wa ugonjwa wa kifua kikuu unafuatia kugunduliwa kwa bakteria wanaoambukiza ugonjwa wa kifua kikuu mnamo Mwaka 1882. WHO linasema Ugonjwa wa kifua kikuu au kwa jina la kitaalamu TB [...]
22/03/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulizi la kigaidi kwenye msikiti mjini Damascus, Syria, ambalo lilifanyika mnamo Machi 21, na kuwaua zaidi ya watu 40, kumjeruhi kiongozi wa kidini na kuwajeruhi watu wengine kadhaa. Katika taarifa ilotolewa na Rais wa Baraza hilo kwa mwezi Machi, Balozi Vitaly Churkin wa Urusi, wanachama wa Baraza hilo wamerejelea azma [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ni hivi karibuni tu shirika la afya duniani WHO lilitoa ripoti inayoonesha kuwa ni mataifa 28 pekee yenye asilimia 7 ya watu wote duniani yana sheria madhubuti za usalama barabarani kwenye maeneo makuu matano ambayo ni kunywa pombe na kuendesha gari, mwendo kasi kupindukia, matumizi ya kofia kwa waendesha pikipiki, kufunga mikanda na matumizi ya [...]
22/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Viongozi na watoa maamuzi barani Afrika, pamoja na wafanyabiashara mashuhuri, wachunguzi wa mambo na wasanii wanatazamia kuanza kukutana Luanda Angola kuanzia tarehe 26 hadi 28 Machi kwa ajili ya kujadili amani. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI YA GEORGE) Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni [...]
22/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema ni vigumu kutokomeza umaskini na kuhakikisha afya nzuri bila maji safi na salama. Akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza Kuu kuhusu ushirikiano kuhsu maji, Bwana Jeremic amesema maji ndicho chanzo cha uhai, na wakati huu wa kuadhimisha mwaka wa kimataifa wa ushirikiano kuhusu maji, [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA , nchini Sudan Kusini , imetoa taarifa kuhusu usalama wa wakazi wa jimbo la Jonglei kufuatia mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikundi vyenye silaha ambapo baadhi ya watu wamejeruhiwa huku wengine wakikimbilia misituni. Katika taarifa yake OCHA imesema watu kadhaa wamekimbia na [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amekaribisha uamuzi wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon kufanya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu madai kwamba huenda silaha za kemikali zimetumiwa nchini Syria. Bi Pillay amesema ofisi ya haki za binadamu i tayari kusaidia katika uchunguzi huo.Hadi sasa hakuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kwamba [...]
22/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC, Fatou Bensouda ameunga mkono taarifa ya kwamba mtuhumiwa wa makosa ya kihalifu huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, Bosco Ntaganda yuko njiani kuelekea makao makuu ya mahakama hiyo mjini The Hague, Uholanzi. Bi. Bensouda amesema leo ni siku nzuri kwa wahanga wa mzozo wa [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya maji hii leo, Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limezishauri serikali, mashirika ya umma na wananchi wa kawaida kutambua kuwa takwimu zozote zinazotolewa, zinajumuisha pia watoto. Mkuu wa kitengo cha maji na usafi ndani ya UNICEF Sanjay Wijesekera, amesema kuna wakati ambapo msisitizo unawekwa kwenye takwimu kubwa [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM limefanikisha kurejeshwa nyumbani salama nchini Uganda kwa watoto watano waliokuwa wamesafirishwa kiharamu kwenda Sudan Kusini. IOM inasema wazazi wa watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 16 waliridhia watoto wao waende Sudan Kusini ili wasomeshwe lakini kinyume chake walikuwa wanatumikishwa kwa kuchuuza bidhaa ndogo ndogo barabarani. [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limelaani na kusikitishwa na shambulio la Alhamisi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mwa Pakistani. Shambulio hilo kwenye kambi ya Jalozai karibu na Peshawar lilisababisha vifo vya watu Kumi na makumi kadhaa wamejeruhiwa ambapo waathirika hao ni pamoja na wakimbizi na wafanyakazi wa kutoa msaada [...]
22/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »