Nyumbani » 21/03/2013 Entries posted on “Machi 21st, 2013”

Hali ya usalama Sudan Kusini bado inatia wasiwasi: UNMISS

Kusikiliza / Hilde Johnson, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UM na Mkuu wa UNMISS

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ujumbe wake nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson, amesema hatua za kuielekeza nchi hiyo kuwa tulivu na imara ni za mwendo usiolingana kote nchini. Akilihutubia Baraza ka Usalama la Umoja wa Mataifa, Bi Johnson amesema ingawa Sudan Kusini imepiga hatua za maendeleo katika sehemu fulani, bado taifa hilo [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasaidia kuwanusuru watoto wakimbizi wa DRC wanaopotea

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Mapigano yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya vikosi vya waasi wa M23 na serikali ya nchi hiyo, yanaendelea kusababisha kadhia kwa raia ambapo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia maswala ya misaada ya kibinadamu OCHA, idadi  ya wakimbizi wa ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni zaidi ya [...]

21/03/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNDP yapokea ripoti ya awali ya maendeleo baada ya 2015

Kusikiliza / undp global conversation

Shirika la Mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, leo limepokea ripoti ya utafiti wa awali kuhusu maoni ya watu mbalimbali juu ya mkakati wa maendeleo baada ya Mpango wa Maendeleo ya Millenia mwaka 2015. Ripoti hiyo iliyochukuliwa katika picha na kupewa jina ''Majadiliano ulimwenguni yaanza"  imehusisha wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 duniani [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Tuupinge ubaguzi wa rangi michezoni: UM

Kusikiliza / racism in sport

Ni nini hasa tunachoweza kukifanya ili kuutokomeza ubaguzi wa rangi? Swali hili wameliuliza wataalam wa ngazi ya juu wa haki za binadamu kuhusu ubaguzi wa rangi kwenye Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi, leo Machi 21. Wataalam hao wamesema siku hii ni muhimu kwa kusherehekea utofauti, na kutoa wito kwa wanamichezo na mamlaka [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia unyanyapaa dunia inapoadhimisha siku ya ugonjwa wa mtindio wa ubongo

Kusikiliza / Mary Queen

Katika kuadhimisha siku ya  mtindio wa ubongo  duniani  ambayo huadhimishwa Machi 21 kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu huo huwanyima nafasi nyingi. Ugonjwa wa mtindio wa ubongo (Down Syndrome) ni hali ya kiasili inayotokea kwa mwili wa mwanadamu inayoathiri uwezo wa kujifunza, tabia za kawaida [...]

21/03/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

FAO yataka kumalizwa ukataji holela wa misitu

Kusikiliza / Ukataji wa miti

Huku Umoja wa Mataifa ukifanya maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya misitu, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Jose Graziano da Silva amezitaka nchi kuunga mkono lengo la kupunguza hadi sufuri ukataji haramu wa miti.  Amesema kuwa kwenye nchi nyingi ukataji wa miti umeathiri viumbe, umesababisha [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban afanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame mjini New York

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais Paul Kagame wa Rwanda

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mjini New York ambapo walizungumzia hali iliyopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo  DRC  kufuatia kutiwa sahihi kwa makubaliano ya amani na usalama kama chombo ya ufumbuzi kwa chanzo cha mizozo katika eneo la maziwa makuu. Wote walikubaliana [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aunda jopo kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametangaza kuunda jopo la kuchunguza madai ya kuwepo kwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.  Bwana Ban amewaeleza waandishi wa habari hii leo kuwa hatua hiyo inafuatia ombi rasmi kutoka mamlaka za Syria la kutaka jopo maalum lisiloegemea upande wowote kuchunguza madai hayo. Katibu Mkuu ametaja [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabianchi yazidi kuwekewa mkakati Tanzania:UM

Kusikiliza / Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal

Wataalamu wa masuala ya tabia nchi, wameanza mkutano wao wa siku tatu nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili njia bora zitakazosaidia kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira.  Mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa kupitia kitengo chake cha sayansi na maridhiano ya pamoja juu ya tabia nchi, kwa kushirikiana na wenyeji Tanzania, utamalizika kwa [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama CAR yazidi kuzorota, Baraza lapaza sauti

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati walioko nchini DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali kuendelea kuzorota kwa usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ambako mapiganop yaliyoanza upya kati ya majeshi ya serikali na waasi wa kundi la Seleka yanatishia usalama wa raia na mpango wa amani uliotiwa saini mapema mwezi Januari mwaka huu. Kauli ya baraza hilo inafuatia [...]

21/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031