Nyumbani » 19/03/2013 Entries posted on “Machi 19th, 2013”

Unicef yapiga kambi Niger kukabiliana na utapiamlo

Kusikiliza / Watendaji wa UNICEF wakitoa tiba kwa wakimbizi wa Mali huko Niger

Mapigano yanayoendelea nchini Mali yamesababisha zaidi ya wakazi 270,000 wa nchi hiyo iliyoko Magharibi mwa Afrika kukimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi. Hata hivyo wakiwa njiani wanakumbana na kadhia mbalimbali na watoto wa wanawake huathirika zaidi.  Nchini Niger, ambako yanapokelewa makundi ya wakimbizi kutoka Mali, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelazimika kupiga [...]

19/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Graziano Da Silva amwakilisha Ban sherehe za kutawazwa Pope Francis

Kusikiliza / Jose' Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu wa FAO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, Jose' Graziano da Silva amehudhuria sherehe za kutawazwa kwa kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis wa I na kusema kuwa Umoja wa Mataifa una matumaini na kiongozi huyo rafiki wa maskini katika kusaidia harakati za kukabiliana na njaa, utapiamlo na ufukara. Graziano da Silva [...]

19/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM na nchi za Caribbean zajadili usalama mipakani

Kusikiliza / Msemaji wa IOM, Jumbe Omari Jumbe

Maafisa kutoka mataifa 11 yaliyoko kwenye ukanda wa Caribbean wameanza kukutana kwa ajili ya kujadilia haja ya kuongeza mashirikiano kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama katika maeneo ya mipakani.  Mkutano huo wa siku mbili ambao umegharimiwa na Marekani unaratibiwa na  IOM. Pamoja na agenda ya uimarishwaji ulinzi na usalama katika maeneo ya mipakani wajumbe [...]

19/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yakaribisha kujisalimisha kwa Bosco Ntaganda

Kusikiliza / MONUSCO DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, umekaribisha kujisalimisha kwa Bosco Ntaganda, na uamuzi wa serikali ya Marekani kumsafirisha hadi The Hague, ambako anatakiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambao anadaiwa kuutenda katika eneo la Ituri kati ya 2001 na [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za kibinadamu ni za kipaumbele katika majukumu yetu Afghanistan: Ban

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wakati taifa la Afghanistan likijiandaa kwa kipindi cha mpito, Umoja wa Mataifa utatakiwa kuchukua hatua za kibinadamu ili kukabiliana na hatari zinazolikabili taifa hilo, na hali inayotokana na kipindi cha mpito. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama hii leo. Akizungumza kuhusu majukumu [...]

19/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yakaribisha tangazo la Papa Francis la kuwajali maskini

Kusikiliza / Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Pope Francis I

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limepongeza mwelekeo mpya ulioanzishwa na Papa Fransis ambaye pamoja na mambo ya imani lakini amesisitiza nia yake ya kuendelea kuwasaidia watu maskani hasa wale walioko Latin Amerika ambako ndiko alikozaliwa. Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin, amesema kuwa WFP amekaribisha hatua ya Papa huyo kuonyesha robo ya ubinadamu [...]

19/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za binadamu yazungumzia kujisalimisha kwa Ntaganda

Kusikiliza / Navi Pillay

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja ya Mataifa imezungumzia taarifa za kujisalimisha kwa Bosco Ntaganda ambaye anadaiwa kuwa kiongozi wa kikundi cha waasi cha M23 huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC na ambaye anatakiwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC. Msemaji wa ofisi hiyo akimkariri mkuu wa Tume Navi Pillay [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wamulikwa: IOM

Kusikiliza / IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Ethiopia wametia sahihi makubaliano ya kutekelezwa kwa mradi wa miaka miwili wenye lengo la kuzuia usafirishaji  haramu wa watu, kuwahakikishia usalama waathirika wa vitendo hivyo na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika nchini Ethiopia. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mjini Addis Ababa ambapo Jumbe Omari Jumbe msemaji wa [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa yaombwa itafute suluhu la mzozo ulio nchini Syria.

Kusikiliza / baridi kali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema taifa la Syria kwa sasa linakabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu huku zaidi ya watu milioni tatu wakilazimika kuhama makwao wakiwemo watu milioni moja wanaotafuta hifadhi katika nchi jirani. Amesema kinachoshuhudiwa kufuatia  hatua zilizochukuliwa na utawala wa Syria kupinga maandamano ya amani yaliyoanza miaka miwili ilopita [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Syria, raia taabani: OCHA

Kusikiliza / Watoto nchini Syria

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu  misaada ya kibinadamu OCHA inasema raia wa Syria ndio wanaingia gharama kutokana na mzozo unaoendelea nchini mwao.  OCHA inasema mzozo huo umefanya watu kupoteza tegemeo lao la maisha, kazi, nyumba, chakula, maji huku wakishuhudia maisha ya baadaye ya watoto wao yakizidi kuhatarishwa. Halikadhalika nyumba, viwanda mitandao ya simu, [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa Yemen

Kusikiliza / Informal Thematic Debate of the 66th Session of the General Assembly on “The Road to Rio+20 and beyond”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya kitaifa nchini Yemen, katika kongamano la siku ya kumbukumbu ya wale walokufa katika maandamano ya amani mnamo Machi 18 mwaka 2011. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema amefurahishwa kuona kuwa mazungumzo hayo yameandaliwa kwa njia ya kina, ni ya [...]

19/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuelekea 2015, nishati mbadala yamulikwa Afrika:UNDP

Kusikiliza / Alberic Kacou, Mwakilishi Mkazi wa UM nchini Tanzania

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP leo limeanzisha majadiliano kwa kanda ya afrika kwa ajili ya kuanzisha msukumo mpya unaotaka kuIngizwa kwa kipengele kinachozingatia nishati mbadala wakati huu wa kuelekea kwenye kilele cha maendeleo ya maendeleo ya milenia, MGDs.  Majadiliano hayo ambayo yamewajumusiha maafisa wa serikali, wachumi, mashirika ya kiraia, yamefanyika jijini Dar [...]

19/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031