Nyumbani » 18/03/2013 Entries posted on “Machi 18th, 2013”

Surua yatishia usalama wa watoto DRC Kongo,UNICEF yasaidia

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC pamoja na mambo mengine yametajwa kukwamisha jitihada za kukabiliana na hatimaye kudhibiti ugonjwa wa surua hususani mongoni mwa watoto.Hii inatokana na kwamba mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi yamesababisha watu kukimbia makazi yao na kuishi katika makzi yenye msongamano .Jitihada za kutoa chanjo zinakwama! [...]

18/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mary Robinson awa Mwakilishi wa Ban kwa nchi za Maziwa Makuu

Kusikiliza / Mary Robinson

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Mkuu wa zamani wa tume ya haki za binadamu ya Umoja huo , Mary Robinson kuwa Mwakilishi wake maalum kwa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika.  Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bi. Robinson atakuwa na dhima ya msingi ya [...]

18/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukata watia hatarini harakati za kudhibiti Kifua Kikuu

Kusikiliza / Mtoto akiwa katika moja ya wodi za tiba dhidi ya Kifua Kikuu huko Phillipines

Shirika la afya duniani WHO na mfuko wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na Malaria yanasema ugonjwa wa kifua kikuu ulio sugu kwa dawa,  unazidi kuenea na kwamba karibu dola bilioni Moja nukta Sita zahitajika kial mwaka kwa tiba dhidi ya ugonjwa huo.  Wakizungumza mjini Geneva kabla ya maadhimisho ya siku [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumaini ya udhibiti wa biashara ya silaha yaelekekezwa New York.

Kusikiliza / Silaha

Mkutano wa mwisho wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kimataifa wa biashara ya silaha umeanza mjini New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ametaka washiriki wa mkutano huo kujikita katika kuangalia madhara yatokanayo na biashara hiyo ambayo amesema ni vyema ikawekewa udhibiti.  Katika hotuba yake kwa washiriki wa mkutano huo utakaomalizika tarehe 28 [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres asifu Albania kupokea wakimbizi wa Iraq

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi, UNHCr, António Guterres, amesema kitendo cha serikali ya Albania kukubali kuwapokea wakimbizi wa Iraq waliokuwa wamehifadhiwa katika kambi ya Hurriya ni hatua ya kutia matumaini na ameipongeza na kuikaribisha.  Albania imekubali kuwapokea wakimbizi hao 210 walikuwa wamehifadhi kwa muda katika kambi ya Hurriya ambayo pia hujulikana [...]

18/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP na UNHCR yapokea msaada kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu

Kusikiliza / Nyarugusu, Kasulu, Kigoma

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la wakimbizi UNHCR na lile la Mpango wa Chakula duniani WFP yamepokea msaada wa Dola Milioni Saba kutoka serikali ya Japan  kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu, Kigoma, magharibi mwa Tanzania. Kambi hiyo ni ya mwisho miongoni mwa kambi zinazohifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Mali wahitaji msaada wa haraka: WFP

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Ertharin Cousin

Wananchi wa Mali wanaendelea kuhangaika baada ya kupoteza makazi yao na kwa sasa wanahitaji haraka msaada wa chakula na misaada mingine ya kibinadamu. Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin aliyoitoa mjini Roma baada ya kuhitimisha ziara yake huko Mali na Burkina Faso. Wakati wa ziara [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Balozi Mahiga alaani shambulio la mjini Mogadishu

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ameeleza kushtushwa na kusikitishwa kwake na shambulio la bomu  lililotokea kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu. Tukio hilo limetokea baada ya gari lililokuwa na vilipukaji kulipuka ambapo taarifa za awali zinadokeza kuwa takribani watu Saba wameuawa na wengine [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu lajadili maeneo ya Wapalestina yalokaliwa

Kusikiliza / Bi Chritine Chanet

Baraza la Haki za Binadamu leo limefanya mazungumzo na tume ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu jinsi haki za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni za Wapalestina katika maeneo yalokaliwa na Waisraeli zinavyoathiriwa, ikiwemo mashariki ya Jerusalem. Mkuu wa tume hiyo, Christine Chanet amesema kuendeleza kazi ya ujenzi kwenye maeneo hayo ni njia moja ya ukoloni ambayo [...]

18/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wamulikwa teknolojia ya mawasiliano baada ya 2015.

Kusikiliza / Mkutano wa Saba wa Makamishna wa Tume ya maendeleo ya digitali ya UM huko Mexico City

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uendelezaji wa teknolojia ya digitali imeweka lengo jipya la kuchochea wanawake kutumia zaidi teknolojia ya habari na mawasiliano, ICT kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanayohusiana na jinsia.  Lengo hilo limewekwa wakati wa mkutano wa Saba wa makamishna wa tume hiyo huko Mexico City, [...]

18/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amsifu Bachelet wakati akiondoka UN WOMEN

michelle-bach2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemsifu Bi Michelle Bachelet kwa kazi yake ilofa wakati akihudumu kwenye wadhfa wa Mkuu wa kitengo cha Wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women. Bi Bachelet ametangaza nia yake kujiuzulu kutoka wadhafa huo mara tu baada ya kumalizika mkutano kuhusu hadhi ya wanawake, ambao umekamilika mjini New [...]

18/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031