Nyumbani » 14/03/2013
Entries posted on “Machi 14th, 2013”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema licha ya kupiga hatua katika kuboresha maisha ya watu, zaidi ya watu bilioni moja bado wanaishi katika umaskini ulokithiri. Bwana Ban amesema hayo wakati wa kufungua kikao cha kundi la kuchukua hatua kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ambapo pia amesema uharibifu wa mazingira unaendelea kuhatarisha [...]
14/03/2013 | Jamii: Malengo ya maendeleo ya milenia, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema linakabiliwa na changamoto kubwa ya kupanua wigo wa operesheni zake za dharura kwa ajili ya mamilioni ya watu walioko katika migogoro mbali mbali duniani. Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Ertharin Cousin amesema wanakumbwa na hali hiyo ikiwemo ukata wakati huu ambapo Syria ambako nako wanapaswa kusaidia, mgogoro wake [...]
14/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema harakati za kubuni malengo ya maendeleo endelevu zitakuwa ngumu, na zitahitaji ustadi mkubwa wa kidiplomasia. Bwana Jeremic amesema hayo wakati wa kufungua kikao cha kwanza cha kundi la Baraza Kuu la kuchukua hatua kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs). Rais huyo wa Baraza Kuu [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga (UNISDR) imesema katika historia na kwa mara ya kwanza kabisa ulimwengu umeshuhudia hasara kubwa ya kiuchumi ya mwaka inayotokana na majanga kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kuzidi dola bilioni 100. Ofisi hiyo imesema tathmini ya hasara ya majanga ya kiasili tangu mwaka [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya ya maendeleo ya wanadamu ya mwaka 2013 inaonyesha mabadiliko makubwa katika mienendo ya maendeleo kote duniani. Mabadiliko hayo yanatokana na kasi kubwa ya kuinuka kimaendeleo kwa nchi zinazoendelea, pamoja na umuhimu wake katika maendeleo ya wanadamu kwa ujumla. Ripoti hiyo inasema kuwa nchi za Kusini mwa ulimwengu zinaendelea kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) kwa kipindi cha miezi kumi na miwili zaidi, pamoja na kulegeza vikwazo vya silaha ili kuiruhusu serikali mpya ya Libya kuweza kuagiza silaha za kutumia katika kuimarisha usalama. Barza la [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwanaufalme wa Uingereza, Prince Charles amepongeza kazi inayofanywa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na washirika wake katika kusaidia maelfu ya wakimbizi wa Syria walio nchini Jordan. Ametoa pongezi hizo alipoitembea kambi moja iliyo kwenye mpaka wa Syria na Jordan kama anavyoelezea Jason Nyakundi. (SAUTI YA JASON)
14/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya papa katika bahari ya Mediteranian na bahari Nyeusi iliyoko kati ya Ulaya Mashariki na bara la Asia imepungua kwa kiasi kikubwa katika karne mbili zilizopita na hivyo kuwa na athari kwa mfumo wa ekolojia ya baharini kwenye maeneo hayo na ule wa ulaji. Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalamu wa haki miliki pamoja na viongozi wa serikali kutoka zaidi ya nchi 20 barani Afrika leo wamehitimisha mkutano wao wa siku tatu jijini Dar es salaam na kutoa wito wa kuundwa sera na sheria kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la wizi wa haki miliki. Mkutano huo ambao pia ulishirikisha baadhi ya wataalamu kutoka [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti mpya inayoonyesha kuwa ni mataifa 28 tu yenye asilimia Saba ya watu wote duniani ambayo yana sheria madhubuti za usalama barabarani kwenye maeneo makuu matano ambayo ni muhimu katika kupunguza ajali za barabarani. Maeneo hayo ni kunywa pombe na kuendesha gari, mwendo kasi kupindukia, matumizi ya kofia kwa [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUSCO umetangaza kujisalimisha kwa askari 10 wa kikundi cha waasi cha M23. Taarifa ya MONUSCO imesema kuwa askari hao wanane ni maafisa polisi wa DRC na wawili ni askari wa Rwanda na walijisalimisha mwezi uliopita kwenye ofisi za ujumbe huo huko [...]
14/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »