Nyumbani » 13/03/2013 Entries posted on “Machi 13th, 2013”

Askari wa Umoja wa Mataifa ajeruhiwa kwa risasi Sudan Kusini

Kusikiliza / askari wa UNMISS wakiwa kwenye doria huko Pibor.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS umelaani shambulizi lililosababisha kujeruhiwa kwa mmoja wa askari wa kulinda amani wakati wa doria Mashariki mwa jimbo la Jonglei nchini humo. Kwa mujibu wa  msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduador del Buey askari huyo alijeruhiwa baada ya kundi la wanajeshi ambalo halikutambuliwa kufyatulia risasi ujumbe wa UNMISS [...]

13/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza uteuzi wa kiongozi mpya wa kanisa Katoliki

Kusikiliza / Kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis I

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametuma salamu za pongezi kwa Kardinali Jorge Mario Bergoglio wa Buenos Aires, Argentina, kwa kuchaguliwa kuongoza kanisa katoliki duniani. Kardinali Bergoglio amechukua jina la Pope Francis wa Kwanza ambapo katika salamu zake, Bwana Ban pia amewapongeza waumini wote wa kanisa katoliki duniani kwa hatua hiyo. Halikadhalika Bwana [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sehemu za ibada zatumika kutoa tiba Uganda: UNICEF

Kusikiliza / Huduma ya afya ikitolewa baada ya ibada nchini Uganda

  Huduma ya afya ya msingi ni jambo muhimu kwa jamii ili waweze kushiriki shughuli za maendeleo. Hata hivyo katika maeneo mengi ya nchi zinazoendelea Uganda ikiwa ni mojawapo, watu hulazimika kwenda mwendo mrefu kupata huduma hizo na hivyo kusababisha kukosa huduma au kuipata wakati wameshachelewa. Kwa mantiki hiyo Shirika la Umoja wa Mataifa la [...]

13/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wakerwa na mauaji ya watu 7 Saudi Arabia

Kusikiliza / torture 2

Wataalam wawili huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yasiyo halali, utesaji na vifungo vya ovyo, leo wameeleza kukerwa na mauaji ya wanaume saba nchini Saudi Arabia, licha ya wito wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya umma wa kuitaka mamlaka ya Saudia  isitekeleze mauaji hayo. Mauaji hayo ambayo yametekelezwa Jumatano asubuhi, yamefanywa kwa kuwapiga [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rushwa ya ngono kikwazo cha maendeleo-Majaji

Kusikiliza / Jaji Engera Mmari-Kileo

Majaji wanaohudhuria mkutano kuhusu hadhi ya wanawake unaoendelea mjini New York, wamesema rushwa ya ngono ambayo ni tatizo kubwa duniani kwa sasa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaochangia kuzorota kwa maendeleo na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi. Mkutano huo umejadili namna ya kutatua ukiukwaji huo wa haki za binadamu unaotajwa pia kushusha viwango [...]

13/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rushwa yapokonya wengi haki za binadamu :Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa hamna shaka kwamba ulaji rushwa ni kizingiti kikubwa katika kuwepo kwa haki za binadamu  zikiwemo za kisiasa , kiuchumi , kijamii , kitamaduni na maendeleo.  Pillay amesema ulaji rushwa unakiuka haki muhimu za kibinadamu zikiwemo za uwazi , uwajibikaji , kutobaguliwa [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kuanzisha mpango mpya kupima uwezekano wa kutokea njaa

Kusikiliza / Mtoto akinyweshwa uji.

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO lipo mbioni kufanya majaribio ya mpango mpya na wa haraka wa kupima tatizo la njaa na ukosefu wa usalama wa chakula.  Taarifa ya FAO inasema mpango huo ulipewa jina la hatua mpya-ya haraka na –ya uhakika, unatazamiwa kuanza kutekelezwa mwezi huu katika nchi za Angola, Ethiopia, Malawi na [...]

13/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliokufa vizuizini DRC 2012 yaongezeka maradufu

Kusikiliza / RIGHTS

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ongezeko kubwa la watu wanaokufa wakiwa kizuizini na magerezani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC hususan katika kipindi cha mwaka jana.  Utafiti huo uliofanywa na ofisi yaTume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini DRC katika vituo kadhaa, umebainisha hali mbaya iliyopo kwenye vituo hivyo [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu mwenendo wa idadi ya watu duniani wamalizika

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa IOM, William Swing

Mkutano wa viongozi wa serikali  kutoka nchi 51 umekamilika leo nchini Bangladesh. Majadiliano ya mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa kwa ushirikiano wa nchi hiyo na Uswisi, yalihusu  mienendo ya  idadi ya watu duniani, likiwemo suala la uhamiaji. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM William Swing aliyeko Bangladesha kwa ziara ya siku [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yasaidia Tume za uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar

Kusikiliza / Alberic Kacou, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limetiliana saini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, NEC na ile ya Zanzibar ZEC, mradi wa kusaidia kura ya maoni kuhusu Katiba mpya mwaka 2014 pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2015. Chini ya mradi huo wa uwezeshaji wa demokrasia, Umoja wa Mataifa utapatia tume [...]

13/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031