Nyumbani » 12/03/2013 Entries posted on “Machi 12th, 2013”

MONUSCO yapambana na waasi DRC Kongo,juhudi zaidi zahitajika

Kusikiliza / MONUSCO

Kongo DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika yenye rasilimali nyingi, ikiwemo madini na uoto wa asili. Nchi hii yenye idadi ya zaidi ya watu milioni sabini ina historia ndefu ya mapigano yaliyosababisha maafa kadhaa ikiwamo vifo, ulemavu na hata wakimbizi wa ndani ya nchi na wale waliokimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi. Mwishoni [...]

12/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban aomboleza vifo vya marubani nchini Kongo DRC.

sgga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepokea kwa masikitiko habari za vifo vya marubani wanne wa Urusi kufuatia ajali ya ndege ya kukodi ya mizigo ya Umoja wa Mataifa iliyoanguka kilometa 20 Mashariki mwa DRC Kongo katika mji wa Kivu Machi 9 mwaka huu. Kufuatia vifo hivyo, Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi na pole [...]

12/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twapongeza makubaliano ya Sudan na Sudan Kusini, sasa watekeleze: UM

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Siku chache baada ya ripoti kuwa Sudan na Sudan Kusini wametia saini makubaliano yenye lengo la kupatia suluhu la kudumu mgogoro wa mpaka kati yao, hii leo pande mbili hizo zimetiliana saini mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mpango wa utekelezaji wa makubaliano tisa kati yao kuhusu masuala mbali mbali ikiwemo mgogoro [...]

12/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Lugha ndogo za asili hatarini kutoweka: Mtaalamu UM

Kusikiliza / human rights council

Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea mjini Geneva, Uswisi kimeelezwa kuwa lugha takribani nusu ya lugha Elfu Sita za makabila madogo duniani ziko hatarini kutoweka mwishoni mwa karne hii kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo sera za kitaifa, muingiliano wa jamii na migogoro ya kivita. Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya [...]

12/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wahitajika kudhibiti wizi wa haki miliki: WIPO

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akiangalia bidhaa za wajasiriamali baada ya ufunguzi wa mkutano wa WIPO, Dar es salaam.

Suala la haki miliki linaelezwa kuwa bado linaendelea kuzua utata na kukwamisha matumizi stahili ambayo yanaweza kusaidia nchi kujikwamua kiuchumi. Barani Afrika ripoti zinaonyesha kuwa mapato mengi hupotea kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa haki miliki, kunafanyika kwenye maeneo mbalimbali. Ni kwa mantiki hiyo wataalamu wanakutana jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa [...]

12/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aonya ongezeko la uvunjifu wa haki za binadamu Iran

Kusikiliza / Ahmed Shaheed

Mtaalamu maamlum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ahmed Shaheed ametoa tahadhari kuhusu idadi ya tuhuma na taarifa anazoendelea kupokea kuhusu hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo akitaka hatua za haraka zichukuliwe. Joseph Msami na maelezo zaidi. (SAUTI YA JOSEPH)

12/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kusaidia bara la afrika kudhibiti Haki miliki

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa WIPO, Francis Gurry na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Haki Miliki, WIPO Francis Gurry leo wameongoza mkutano kuhusu hakimiliki jijini DSM ukishirikisha wataalamu na viongozi wa serikali na sekta binafsi kutoka zaidi ya nchi 20 barani Afrika kwa ajili ya kujadilia njia bora za kukabiliana na wizi wa haki [...]

12/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Syria unakiweka kizazi kizima cha watoto mashakani: UNICEF

Kusikiliza / watoto, Syria

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeonya kuwa kizazi kizima cha watoto wa Syria kipo mashakani, wakati mzozo wa Syria ukiingia mwaka wa tatu. Katika ripoti yake ilotolewa leo ambayo ni tarehe ya kutimu miaka miwili tangu mzozo wa Syria kuanza, UNICEF imesema kuwa kukithiri kwa machafuko, uharibifu mkubwa wa miundo mbinu [...]

12/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria Uturuki yaongezeka: Guterres atembelea kambi

Kusikiliza / Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres akiwa katika kambi moja huko Uturuki

Idadi ya raia wa Syria walio wakimbizi nchini Uturuki kwa sasa imefikia zaidi ya Laki Mbili na Nusu baada ya serikali kuanza kuwaandikisha pamoja na wale walio nje ya kambi 17 zinazosimamiwa na serikali. Taarifa hiyo zinajiri huku mkuu wa Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres akiwa ziarani nchi jirani [...]

12/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uvamizi kaskazini mwa Mali umekiuka haki za kijamii, kitamaduni na kiuchumi: Ripoti

Kusikiliza / raia wa Mali

Naibu Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang ametoa ripoti yake kuhusu hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Mali na kueleza kuwa hali ni ya kutisha ambapo waasi wa kikundi cha MNLA walifanya mauaji ya raia kwa minajili ya tafsiri ya sheria ya kiislamu, Sharia.  Ripoti [...]

12/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yatoa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa polisi wa kike

Kusikiliza / Maandamano siku ya Wanawake huko Juba.

Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya wanawake Machi Nane ambapo tumeshuhudia maadhimisho hayo yakifanyika kwa matukio mbalimbali ikiwemo matembezi na kadhalika, nchini Sudan Kusini,Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, umetumia maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kufundisha  Kiingereza  wanawake zaidi ya 50.  Mafunzo hayo yanafanyika katika hema lililoko katika karakana iliyoko katika kituo cha [...]

12/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031