Nyumbani » 11/03/2013 Entries posted on “Machi 11th, 2013”

Wakimbizi waliorejea nyumbani Liberia kuwezeshwa: UNIDO

Kusikiliza / Wakimbizi wa Liberia wakati wa kurejeshwa nyumbani

Katika kuhakikisha wakimbizi wa Liberia waliorejea nyumbani wanatangamana vizuri na maisha ya kila siku, Shirika la umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO limeandaa miradi inayolenga kuwapatia wakimbizi hao mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali. Taarifa ya UNIDO imemkariri Mkuu wa kitengo cha teknolojia ya kilimo na viwanda Chakib Jenane akisema kuwa idadi kubwa [...]

11/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO yahamasisha Uganda iendeleze kilimo cha biashara

Kusikiliza / Graziano Da Silva

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula duniani, FAO José Graziano da Silva amesifu serikali ya Uganda kwa uongozi wake thabiti wa kuimarisha sekta ya kilimo na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. Da Silva Ametoa pongezi hizi wakati wa ziara yake ya siku moja nchini humo ambapo alikuwa na mazungumzo na Makamu [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni wakabiliwa na njaa Malawi-FAO

Mahindi yakiwa yameanikwa nchini Malawi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema licha ya kwamba Malawi imepiga hatua katika uzalishaji wa mahindi, uhakika wa chakula na hata kusafirisha nje nafaka hiyo bado watu milioni mbili nchini humo hawana uhakika wa chakula. Mkurugenzi huyo mkuu wa FAO na Kamishna wa Maendeleo ya Umoja [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yajiandaa kwa uchaguzi mkuu, Ban atoa ujumbe

Kusikiliza / Wachuuzi katika soko kuu mjini Bujumbura, Burundi

Nchini Burundi, harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zimeanza na tayari ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi, BNUB imeitisha kikao cha wanasiasa nchini humo kinachonuwia kumaliza uhasama na kuandaa  vema uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015. Kikao hicho kinawakutanisha wanasiasa wa chama tawala pamoja na wale wa upinzani ambao baadhi yao wamerejea [...]

11/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban asifu makubaliano mapya ya mpaka kati ya Sudani na Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameyakarikibisha makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini yenye lengo la kuimarisha usalama wa mpaka ambayo yatasaidia kupatia ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa mpaka kati ya nchi mbili hizo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, makubaliano hayo yanahusu [...]

11/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaitaka Zimbabwe ilinde watoto dhidi ya madhara ya kisiasa

Kusikiliza / Anthony Lake, Mkurugenzi Mtendaji UNICEF

Shirika la kuhudumiwa watoto duniani, UNICEF limeitaka Zimbabwe kulinda watoto wakati taifa hilo linaelekea katika kupiga kura ya maoni kuhusu katiba na uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu. Katika ziara yake ya siku mbili nchini humo Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony Lake pamoja na kuitakia amani Zimbabwe katika shughuli hizo, amesema ni jukumu la kila mmoja [...]

11/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tume huru ta UM kuhusu hali nchini Syria yatoa taarifa yake.

Kusikiliza / Paulo Sérgio Pinheiro

Tume huru ya kimataifa inayoendesha uchunguzi kuhusu Syria imesema kuwa taifa hilo linaendelea kuzama kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.  Akihutubia kikao cha Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Sérgio Pinheiro amesema sababu kuu ya kuwepo vifo vingi , kuhama kwa watu na uharibifu [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukaji wa haki za binadamu Korea Kaskazini umekithiri: Mtaalam wa UM

Kusikiliza / Bendera ya Korea Kaskazini

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Korea Kaskazini (DPRK), Marzuki Darusman, amesema kuna aina tisa tofauti za mienendo ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Korea Kaskazini (DPRK), na ambayo imerekodiwa katika daftari za Umoja wa Mataifa. Akilihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva Uswisi, ambako [...]

11/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanasiasa wajadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu Burundi: UM

Kusikiliza / Uchaguzi mkuu nchini Burundi mwaka 2010

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi, BNUB imeitisha kikao cha wanasiasa nchini humo kinachonuwia kumaliza uhasama na kuandaa  vema uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015. Kikao hicho kinawaleta  kwa pamoja wanasiasa walio karibu na chama tawala pamoja na wanasiasa wa upinzani ambao baadhi yao wamerejea nchini  wiki iliyopita. Katika mkutano huo wanasiasa hao wanajadili [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miaka miwili baada ya ajali ya Fukushima, IAEA yahakikisha usalama wa nyuklia

Kusikiliza / Jopo la wataalamu wa IAEA wakikagua mtambo wa Fukushima Daiichi mwezi Mei mwaka 2011

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki  IAEA Yukiya Amano amesema miaka miwili baada ya tsunami nchini Japani lililosababisha ajali katika mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi nchini humo, shirika lake linaendelea kushirikiana na nchi hiyo kuimarisha usalama kwenye mitambo.  Ametoa tamko hilo leo ikiwa ni kumbukumbu ya miaka miwili tangu tetemeko [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yatupilia mbali mashtaka dhidi ya Muthaura

Kusikiliza / Fatou Bensouda

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC ya huko The Hague, Fatou Bensouda ametangaza kufuta mashtaka dhidi ya mtuhumiwa wa kesi ya vurugu zilizoibuka nchini Kenya baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007, Francis Muthaura. Akitangaza uamuzi wake huo hii leo, Bensouda amesema ameuchukuwa kwa uangalifu mkubwa na kwamba ni wajibu wake [...]

11/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031