Nyumbani » 08/03/2013 Entries posted on “Machi 8th, 2013”

Majeshi ya Burundi yakomboa wananchi kwa kutoa tiba nchini Somali

Kusikiliza / Somalia health

Wiki hii Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalai (AMISOM) ambao umekasimiwa mamlaka na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatimiza maadhimisho ya sita tangu uwasili nchini Somalia huku ukikabiliwa na changamoto mbalimbali lakini pia maadhimisho hayo yakitaja baadhi ya mafanikio kama vile kuimarika kwa usalama na huduma za afya. Licha ya usalama kuimarika [...]

08/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi wa serikali DRC walotekeleza uhalifu waadhibiwe: MONUSCO

Kusikiliza / MONUSCO DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUSCO), umesema kwamba umepokea maelezo yanayoonyesha kuhusika kwa vikosi vya serikali (FARDC) katika vitendo vya ubakaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu mnamo mwezi Novemba mwaka 2012. Maelezo haya yametokana na uchunguzi ulofanywa na ujumbe wa haki za binadamu kwenye mji wa Minova [...]

08/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tafiti zaidi zahitajika kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia: TAMWA

Kusikiliza / Stop violence

Siku ya wanawake duniani ni fursa ya kutathmini hatua zilizochukuliwa kulinda hadhi na ustawi wa mwanamke na mtoto wa kike. Nchini Tanzania, chama cha waandishi wa habari wanawake, TAMWA kiliendesha utafiti kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia, utafiti uliofanyika katika wilaya Kumi nchini humo. Je nini kilibainika? Na matokeo ya utafiti huo yanalenga kuboresha nini? [...]

08/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Yatosha, sasa tuchukue hatua kulinda mwanamke na mtoto wa kike:UM

Kusikiliza / Mkutano maalum, "Ahadi ni Ahadi" makao makuu ya UM mjini New York, Marekani.

Machi Nane ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambapo lengo ni kumulika utekelezaji wa haki za wanawake kwa kuzingatia kuwa tayari kuna mkataba wa kimataifa wa kupinga vitendo vyovyote vya ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW. Mwaka huu tochi inamulika zaidi vitendo vya ukatili, majumbani, makazini, sehemu za biashara, kwenye migogoro na [...]

08/03/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria zipo lakini hazijitoshelezi: UN Women Tanzania

Kusikiliza / Mwanamke wa kitanzania akiwa shambani

Nchini Tanzania, afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN-Women, Fortunata Temu ametaja ukatili wa majumbani kuwa miongoni mwa ukatili unaomkumba mwanamke wa kitanzania ambapo unahusisha vipigo, kutukanwa na kunyanyaswa. Amesema sheria zipo lakini hazitoshelezi. (SAUTI  Fortunata)

08/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari 21 wa UNDOF wako salama: Ladsous

Kusikiliza / Hervé Ladsous

Msimamizi mkuu wa shughuli za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous amelieleza baraza la Usalama kuhusu hali ya walinzi wa amani 21 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo kwenye maeneo huru ya uangalizi, UNDOF huko Golan, ni salama na kwamba jitihada zinaendelea ili waweze kuachiwa huru.  Akitoa muhtasari kwa [...]

08/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi wahama makwao nchini Syria: WFP

Kusikiliza / Watoto Syria

  Mapigano yanayoendelea kushuhudiwa kwenye jimbo la Raqqah kaskazini mashariki mwa Syria yamechangia kuhama kwa watu upya wakati zaidi ya familia 20,000 zinapohama makwao na kukimbila jimbo la Deir Ezzor. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetuma malori matatu yaliyosheheni chakula kwa watu 20,000 kwa muda wa siku tatu zilizopita kitakachosambazwa kwa familia zilizohama [...]

08/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tukomeshe aina zote za ukatili dhidi ya wanawake: UN WOMEN

Kusikiliza / Maandamano siku ya wanawake duniani

Mkuu wa kitengo cha masuala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, ametoa wito kwa serikali kote duniani zisikubali kuiachia mivutano na hali ya kusita sita kuzuia hatua za kuendeleza hadhi ya wanawake duniani. Katika ujumbe wake kwenye siku hii ya kimataifa ya Wanawake, (Bi Bachelet amesema wakati siku hii ikiadhimishwa mwaka huu, wawakilishi [...]

08/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi wa angani wabaini kuzorota kwa usalama huko Kivu Kaskazini: IOM

Kusikiliza / Wakazi katika eneo la Kitchanga, jimbo la Kivu Kaskazini, DRC

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema watu 75,000 wamekimbia makazi yao kwenye jimbo la Kivu Kaskazini huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC kufuatia mapigano yaliyoubuka hivi karibuni katika eneo la Kitchanga, lililopo karibu na mji wa Masisi, takribani kilomita 80 magharibi mwa mji wa Goma.  Taarifa hizo ni kwa mujibu wa [...]

08/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kumwezesha mwanamke kutanufaisha dunia nzima: IMF

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Christine Lagarde

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF, Christine Lagarde amesema kuwa iwapo wanawake watapatiwa fursa ya kutumia kikamilifu vipaji vyao, basi siyo wao tu watakaofaidika, bali ni dunia nzima.Amesema kuwa wanawake wameendelea kukabiliwa na vizingiti vingi, vingine ambavyo baadhi yao vinawanyima uhuru wa kuchagua maisha wayapendayo. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI YA GEORGE) [...]

08/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitendo sasa vyahitajika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-Moon katika shughuli maalum ya siku ya wanawake duniani, "Ahadi ni Ahadi".

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani hii leo na kutaka kila mtu kwa nafasi yake kusongesha mbele jitihada za kimataifa za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike ili kundi hili liweze kuishi huru na katika mazingira salama na yenye ulinzi. Bwana Ban amesema [...]

08/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili kwa wanawake wahusiana na uhakika wa chakula: Mashirika UM

Kusikiliza / Mwanamke akiwa shambani na mwanae mgongoni

Wakati leo ni siku ya wanawake duniani, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula kwa pamoja yametoa taarifa yakiweka bayana uhusiano kati ya ukatili wanaofanyiwa wanawake na uhakika wa chakula. Mashirika hayo lile la chakula na kilimo, FAO, maendeleo ya kilimo na chakula IFAD, mpango wa chakula duniani, WFP pamoja na shirika la kimataifa [...]

08/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031