Nyumbani » 07/03/2013 Entries posted on “Machi 7th, 2013”

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari wa radio nchini Brazil

Kusikiliza / Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Brazil  Mafaldo Bezzera Goes aliyeuwawa kwa kipigwa risasi.  Bibi Bokova katikaa tamko hilo la kulani mauaji ya mwandishi Mafaldo,ametaka uchunguzi wa kina juu ya mauaji hayo ufanyike na wauaji wafikishwe katika vyombo [...]

07/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yatoa elimu juu ya kazi na wajibu wa ujumbe huo Sudan Kusini

Kusikiliza / unmis-logo-gde

Katika kutoa elimu juu ya wajibu na majukumu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) katika jamii ya jimbo la Jonglei, ujumbe huo ulizuru jamii ya watu wa AKUIDENG BOMA, mji ulioko Jalle Payam takribani kilometer 60 kutoka mji unaofahamika kama Bor. Ungana na Joseph Msami katika makala hii inayomulika juhudi za UNMISS [...]

07/03/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uhusiano kati ya mazingira na haki za binadamu ni dhahiri

Kusikiliza / maendeleo ya viwanda na uchafuzi wa mazingira

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mazingira, John Knox amesema kuna umuhimu wa haraka wa kufafanua ni jinsi gani haki za binadamu zinahusiana na kufurahia mazingira safi, huru na salama. Katika ripoti yake mbele ya Baraza la haki za binadamu, Knox amesema ufafanuzi huo ni muhimu ili serikali na taasisi [...]

07/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ndoa za watoto zaidi ya milioni 140 kufanyika kati ya 2010 na 2020: UNFPA

Kusikiliza / Mtoto aliyeozwa akiwa mdogo

Kati ya mwaka 2011 na 2020, zaidi ya watoto milioni 140 wataingizwa kwenye ndoa za watoto, kwa mujibu wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaohusika na idadi ya watu, UNFPA. Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na UNFPA, pamoja na Shirika la Kuhudumia Watoto la UNICEF na Shirika la Afya Duniani, WHO, ikiwa viwango vya sasa [...]

07/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Licha ya maendeleo ya kisiasa janga la misaada ya kibinadamu ni tishio Yemen

Kusikiliza / yemenidp1

Kundi la Misaada ya Kibinadamu nchini Yemen limehadharisha kwamba ikiwa hatua za dharura juu ya misaada ya kibinadamu hazitachukuliwa nchini humo, hakutakuwa na hatua za kimaendeleo. Hadhari hiyo inatolewa wakati ambapo marafiki wa Yemen wanakutana mjini London, Uingereza kujadili hali ya kisiasa, kiuchumi na usalama wa nchi hiyo iliyoko kwenye kipindi cha mpito. Mwakilishi Mkazi [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto walindwe dhidi ya ukatili wa kingono

Kusikiliza / Marta Santos Pais

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, Marta Santos Pais amesema katika nchi zaidi ya80 duniani hivi sasa kuna ajenda za kudhibiti ukatili dhidi ya watoto, zaidi ya nchi 30 zina sheria za kulinda ukatili huo na kuna ongezeko la tafiti za kubaini ukubwa wa tatizo. Hata hivyo amesema [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aunga mkono vikwazo dhidi ya DPRK

Kusikiliza / ban-ki1

Katika taarifa ambayo ameitoa mara tu baada ya kura ya Baraza la Usalama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha azimio hilo na kusema ya kwamba, kwa kulipitisha kwa kauli moja, Baraza la Usalama linatuma ujumbe kinaga ubaga kwa DPRK ya kwamba, jamii ya kimataifa haitokubali juhudi zake za kuendeleza silaha za kinyuklia [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laiwekea DPRK vikwazo

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio nambari 2094 la mwaka 2013, likilaani vikali jaribio la nyuklia lililotekelezwa na Jamhuri ya Korea Kaskazini,  DPRK tarehe 12 Februari, na kuiwekea upya vikwazo vikali, chini ya aya ya saba ya Mkataba Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Halikadhalika azimio hilo linaiwekea DPRK [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa DRC wapaza sauti vita ikomeshwe

Kusikiliza / Baadhi ya washiriki katika kikao cha 57 cha Kamati ya Hadhi ya wanawake.

Wakati dunia inaelekea katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwanamke, baadhi ya wanawake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC wanaoshiriki mikutano ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kuhusu hali ya mwanamke, wamepaza sauti zao na kusema kuwa vita mashariki mwa nchi hiyo sasa basi kwani vinazidi kumgandamiza mwanamke na kumfanya ashindwe [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uvunaji wa zao la ngano watazimiwa kuongezeka mwaka 2013

Kusikiliza / Zaola ngano

  Uvunaji wa zao la ngano katika kipindi cha mwaka 2013,inatazamiwa kuongezeka na kufikia tani milioni 690 ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.3 ikilinganishwa na mwaka uliopita huku mapigano katika baadhi ya nchi yakiripotiwa kukwamisha uhakika wa chakula.   Takwimu zilizotolewa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO zinaonyesha kiwango cha mavuno kinatazamiwa kuongezeka zaidi [...]

07/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kila mtoto ana haki ya kupata huduma bora ya afya: UM

Kusikiliza / Watoto nchini Haiti wakipatiwa huduma ya afya ya kinywa

Kamishina mkuu wa haki za binadfamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema haki ya afya ni haki ya msingi ya binadamu inayotambuliwa na mkataba wa kimataifa wa mtoto ambao unataka kila nchi ichukue hatua kupunguza vifo vya watoto na kufutilia mbali mambo yoyote yanayomdhuru mtoto.  Akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu huko Geneva [...]

07/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Mali huko Niger waendelea na elimu ya msingi

Watoto wa Mali wanaoishi katika kambi ya Mangaize nchini Niger

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na washirika wake limewezesha zaidi ya wakimbizi watoto Elfu Nne Mia Saba wa Mali walioko nchini Niger kuendelea na elimu ya msingi kwenye kambi mbali mbali nchini humo wakati huu ambapo Mali iko katika mgogoro.  Chini ya ushirikiano huo, vifaa vya shule pamoja na mahema [...]

07/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031