Nyumbani » 06/03/2013 Entries posted on “Machi 6th, 2013”

Watu kutoweka katika mazingira tata bado ni tatizo duniani: De Frouville

Kusikiliza / Olivier De Frouville

Mwenyekiti wa kikundi cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na udhibiti wa vitendo vya watu kutoweka katika mazingira tatanishi Olivier De Frouville amesema matukio ya watoto kutoweka katika mazingira hayo ni mojawapo ya vitendo vibaya zaidi vya ukatili dhidi ya watoto. Katika taarifa yake aliyoitoa mjini Geneva, Uswisi, De Frouville amesema kwa kuzingatia kuwa kutoweka katika [...]

06/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNDOF waachiwe mara moja: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama la UM, Balozi Vitaly Churkin

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja wamelaani vikali kitendo cha wapinzani wenye silaha wa  Syria cha kuwashikilia kuanzia jumatano asubuhi kundi la zaidi ya askari 20 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo kwenye maeneo huru ya uangalizi, UNDOF.  Akisoma taarifa ya wajumbe hao mbele ya waandishi wa [...]

06/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Majanga yatokanayo na maji yanaathiri kila nchi: Jeremić

Kusikiliza / Mafuriko Msumbiji

  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremić amesema majanga yatokanayo na maji yameendelea kusababisha madhara kwa nchi mbali mbali duniani, ziwe maskini au tajiri huku akiweka bayana kuwa nchi maskini zinabeba mzigo zaidi wakati wa kukabiliana na hali hiyo. Akizungumza katika kikao maalum cha baraza hilo kuhusu majanga yatokanayo na maji, [...]

06/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNMISS yatoa ulinzi kwa raia waliokimbilia ofisi yake Sudan Kusini

Kusikiliza / Raia akitafuta hifadhi kwenye eneo eneo la UNMISS

Zaidi ya watu 2,500 wamekimbilia makao ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) Jumatano asubuhi kufuatia mapigano yalozuka kati ya kundi moja lenye silaha na wanajeshi wa serikali, SPLA, karibu na soko la Pibor, kwenye jimbo la Jonglei.  Kwa kuitikia matukio hayo, UNMISS imewatuma wanajeshi wake wa kulinda amani kusaidia kuwalinda raia katika [...]

06/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

AMISOM yaongezewa muda hadi mwakani

Kusikiliza / AMISOM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha mswada wa azimio nambari 2093, ambalo linaongeza muda wa kuhudumu wa vikosi vya Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, hadi Februari 28 mwaka 2014. Pamoja na hayo, azimio hilo pia linaiondolea nchi hiyo ya Pembe ya Afrika vikwazo vya silaha za kijeshi. Akiongea [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakenya hitimisheni uchaguzi kwa amani: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Wakati raia wa Kenya wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kukamilisha shughuli za uchaguzi kwa amani na njia inayoaminika itakuwa hatua muhimu katika demokrasia ya Kenya. Bwana Ban amesema kwamba ametiwa moyo kuona shughuli ya uchaguzi ikiendeshwa kwa njia ya amani na [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya kufanya kazi ni ya wote: Pillay

Kusikiliza / Watu wenye ulemavu wakiwa kazini

  Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa haki ya kufanya kazi ni haki iliyo muhimu lakini mamilioni ya watu walio na ulemavu kote duniani wanaendelea kunyimwa haki hiyo na pia kunyimwa fursa ya kushiriki kwenye ujenzi wa jamii zao. Pillay amesema kuwa kuna changamoto tatu ambazo mara [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wa kipalestina huko Israel wahakikishiwe usalama: UNICEF

Kusikiliza / Shirika la kuhudumia watoto la UM, UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limetoa mpangilio wa hatua ambazo zitachukuliwa ili kuboresha hali ya watoto wa kipalestina wanaozuiliwa na jeshi la Israel. Kupitia kwa taarifa yenye kichwa "watoto walio kwenye kizuizi cha jeshi la Israel" UNICEF inapendekeza kutendewa  vyema watoto kipalestina walio kwenye kuzuizi cha jeshi la Isael kuambatana na viwango [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya Tembo Afrika mashakani: Ripoti mpya

Kusikiliza / Askari akisimamia uteketezaji wa pembe za ndovu

Kumekuwa na wasiwasi wa kuendelea kupotea kwa idadi kubwa ya tembo barani Afrika kutokana ongezeko kubwa la biashara ya magendo ya pembe za ndovu. Ripoti mpya iitwayo " Tembo waliogizani- Tembo wa Afrika Mashakani" imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la uwindaji haramu unaoshuhudiwa katika maeneo ya Afrika ya Kati hadi maeneo mengine ikiwemo Mashariki na [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria wafikia Milioni Moja: UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria

Idadi ya raia wa Syria walio wakimbizi wa ndani na wa nje imeongezeka na kufikia milioni Moja, na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amesema idadi hiyo inaongezeka na kwamba wasyria wanaovuka mpaka inaongezeka kila siku. Guterres amesema hali ya Syria [...]

06/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuendeleza ushirikiano na Venezuela

Kusikiliza / Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, enzi za uhai wake akihutubia Baraza Kuu la UM mjini New York, Marekani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesisitiza tena kuwa Umoja huo utaendelea kuunga mkono jitihada za Venezuela za maendeleo na ustawi. Bwana Ban amesema hayo katika salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Hugo Chavez.  Katika salamu hizo pamoja na kuelezea kushtushwa na kifo cha Rais Chavez, Bwana Ban [...]

06/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930