Nyumbani » 05/03/2013 Entries posted on “Machi 5th, 2013”

Ban atuma rambi rambi zake kufuatia kifo cha Chavez

Kusikiliza / Marehemu Chavez

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametuma ujumbe wa rambi rambi kwa familia na watu wa Venezuela kufuatia kifo cha rais wao, Hugo Chavez. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Bwana Ban ambaye amekiri ya kwamba ndio kwanza alikuwa anasikia habari za kifo cha Chavez katika mkutano huo nao, amemsifu Marehemu [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awasihi Wakenya kukamilisha kura kwa amani

Kusikiliza / Ban Akikutana na waandishi wa habari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa watu wa Kenya kulinda amani na kutoa nafasi ya kumalizika kwa shughuli ya uchaguzi nchini humo kwa njia ya kuaminika, wakati huu wanaposubiri kumalizika kuhesabiwa kwa kura, kinyume na mambo yalivyokuwa mwaka 2007. Bwana Ban amewaambia waandishi wa habari mjini Neww York kwamba ametiwa [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latakiwa kuruhusu jeshi la kulinda amani Drc Kongo

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kuruhusu jeshi la kulinda amani ili kusaidia kurejesha hali ya utulivu Mashraiki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Huo ni wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon wakati akihutubia baraza hilo mapema Jumanne. Amesema hali katika eneo hilo ni mbaya ambapo maelfu ya [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake hunipa uchungu: Ban

Kusikiliza / Informal Thematic Debate of the 66th Session of the General Assembly on “The Road to Rio+20 and beyond”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni jambo ambalo humpa uchungu sana, akiongeza kuwa ndiyo maana amejitolea kuona kuwa mtandao wa viongozi wa kiume wanaopinga ukatili na kuwadhalimu wanawake unapanuka. Akihutubia hafla ilofanyika pembezoni mwa mkutano wa tume inayohusika na masuala ya wanawake unaoendelea kwenye ukumbi [...]

05/03/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatua zichukuliwe kutokomeza dhuluma dhidi ya wanawake: UN Women

Kusikiliza / Michelle Bachelet 2

Katika ujumbe wake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Kitengo cha Wanawake katika Umoja wa Mataifa, (UN WOMEN) Michelle Bachelet, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutimiza ahadi zake na kulinda haki ya wanawake kuishi bila kudhulumiwa. Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu inakuja wakati mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali [...]

05/03/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za binadamu lajadili raia kuwekwa vizuizini ovyo na mapambano dhidi ya ugaidi

Kusikiliza / arbitray detention

Baraza la Haki za Binadamu limekuwa na majadiliano  muhimu na Mads Andenas kutoka kundi la kuchukua hatua kuhusu haki za kuwekwa vizuizini ovyo, na Ben Emmerson, ambaye ni mataalamu maalum wa kutetea na kulinda haki za binadamu katika mapambano dhidi ya ugaidi. Katika majadiliano kuhusu haki za kuwekwa kizuizini, wanenaji wamesema mfululizo wa matukio ya [...]

05/03/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

EU na FAO zaapa kuunga mkono juhudi za kuhakikisha lishe na usalama wa chakula Malawi

Kusikiliza / Lishe kwa watoto nchini Malawi

Rais wa Malawi Joyce Banda amekuwa na mazungumzo na Kamishna wa Maendeleo ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Andris Piebalgs, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva, juu ya kukabiliana na tatizo la lishe na ukosefu wa chakula matatizo ambayo yanaendelea kuliandama taifa hilo.   Watendaji hao wa [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ashutumu mauwaji wa walemavu wa ngozi Tanzania, ataka wahusika wachukuliwe hatua.

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za binadamu Navy Pillay ameitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua za hataka kukomesha vitendo vya mauwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi. Amesema kuwa amevunjwa moyo na kusikitishwa juu ya taarifa za kukithiri kwa mauwaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, na hivyo kutoa mwito kwa serikali [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na washirika wazuru Sudan,wabaini hali tete za afya kwa maelfu ya raia.

Kusikiliza / south sudan blue nile

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi na misaaada ya kibinadamau kwa kushirikiana na mwakilishi wa serikali ya Uingereza wamefanya ziara katika maeneo ya wazi katika mji mkuu wa Sudan Khartoum ambako maelfu ya raia wa Sudan Kusini wakipokezana malazi wakati wanasubiri kurejea nyumbani.  Mashirika hayo yanaoyoongozwa na Shirika la Umoja wa Mataifaifa la Uhamiaji, [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Theluthi mbili ya wanaokabiliwa na hatari ya mabomu ya ardhini nchini Mali ni watoto.: UNICEF

Kusikiliza / Wanawake nchini Mali wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapimwe afya

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetahadharisha kuhusu hatari inayozikumba jamii kati na kaskazini mwa Mali,  hatari inayotokana na risasi na mabomu ya ardhini. Tangu mwezi Aprili mwaka uliopita visa 60 vinavyohusiana na mabomu ya ardhini vimeripotiwa huku visa  miongoni mwa watoto vikichukua theluthi mbili ya visa vyote. Kati ya visa hivyo [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yafutilia mbali awamu ya tatu ya mbio za Marathon ukanda wa Gaza

Kusikiliza / Mbio za Gaza Marathon 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limefutilia mbali awamu ya tatu ya mbio za masafa marefu ambazo zingeandaliwa tarehe kumi mwezi Aprili mwaka huu. Hatua hii ya kuvunja moyo inajiri baada ya mazungumzo na utawala kwenye ukanda wa Gaza ulioshikilia msimamo wa kutotaka wanawake washiriki kwenye mbio hizo. Hata hivyo [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatoa ombi la dola miloni 70 zaidi kwa oparesheni zake eneo la maziwa makuu

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa ombi la dola milioni 70 zaidi kwa oparesheni zake mwaka 2013 kuwasaidia maelefu ya raia waliolazimika kuhama makwao katika eneo la maziwa makuu. Fedha hizo ni kwa wale waliohama makwao kutokana na mzozo ulioshuhudiwa kwenye mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi [...]

05/03/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031