WIPO yapanua kumbukumbu zake za nembo za biashara na Hakimiliki

Kusikiliza /

WIPO

Shirika la kimataifa linalohusika na kulinda nembo za biashara na hakimiliki, WIPO limetangaza kupanuka kwa kumbukumbu zake za nembo na majina ya biashara.

Shirika hilo limejumuisha kwenye kumbukumbu zake sehemu zingine sita ikiwemo ofisi ya majina na nembo za bishara nchini Marekani  na kuongeza kumbukumbu zake kutoka milioni 2.2 hadi milioni 10.9 na kulifanya kuwa Shirika kubwa zadi duniani linalowaweza watu kufanya utafiti na kutafuta majina ya biashara na nembo bila malipo

Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry anasema kuwa mfumo wa sasa unaowawezesha wafanyibiashara kutafuta nembo na majina ya biashara sasa ni wa bure.

Ameutaja mfumo huo kama jitihada za kuuunganisha ulimwengu na kumuwezesha kila mmoja aliye popote pale ulimwenguni na habari za kutosha kuhusu uandikishaji wa biashara.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031