WFP yasafirisha misaada ya chakula kwenda Punia mashariki mwa DRC

Kusikiliza /

Ndege ikiwa na shehena ya misaada

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesafirisha kwa ndege vyakula kwa ajili ya maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kwenye mji wa Punia ulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC. WFP imesema usambazaji wa biskuti zenye lishe bora unatarajiwa kung'oa nanga hapo kesho.

Shirika hilo limesema mvua kubwa zinazonyesha zimelazimu watumie ndege kwa kuwa malori ya mizigo hayawezi kupita katika barabara.

WFP imesema karibu tani 20 za chakula kilichosafirishwa kutoka mjini Goma kwa muda wa siku mbili zilizopita kitatumika kuwalisha watu 40,000 sehemu za vijijini.

Katika hatua nyingine, WFP imesema licha ya kwamba inaendelea na mgao wa misaada huko Mali, bado usalama ni tatizo eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA BYRS

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031