Wataalamu wa UM wataka uchunguzi kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu Korea Kaskazini

Kusikiliza /

Bendera ya Korea Kaskazini

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu limesema kuwa, kuna haja ya kutambua na kuweka msukumo juu ya utekelezwaji wa mapendekezo ya kuendesha uchunguzi, ili kubaini tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Korea ya Kaskazini.

Kundi hilo limesisitiza haja ya kuendesha uchunguzi huo ili kubainisha ukweli wa mambo, hasa kutokana na madai ya kubinywa kwa wanasiasa na wengine wanaoendelea kutumikia vifungo vya kisiasa.

Korea Kaskazini inadaiwa kuanzisha makambi ambayo inahifadhi wafungwa wa kisiasa na baadhi ya familia za wafungwa hao ziko taabani.

Kundi hilo la wataalamu limezitolea mwito nchini wanachama wa Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi huru kuhusiana na tuhuma hizo, likisema kuwa, kuundwa kwa tume hiyo kutasaidia kufichua ukweli wa mambo

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031