Wakimbizi Mogadishu wahamishiwa makazi mapya: UM

Kusikiliza /

Mtoto akiwa ndani ya moja ya kibanda ambacho ni makazi yao huko Somalia

Maisha duni ya wakimbizi wa ndani mjini Mogadishu Somalia yaliyodumu kwa takribani miongo miwili ya mzozo nchini humo sasa yameimarika kutokana na hatua zilizochukuliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Mashirika hayo 14 pamoja na mengine ya kiraia yalichukua hatua ya kuhamisha familia Elfu Tano za wakimbizi kwenda maeneo mapya mjini Mogadishu ambako makazi, malazi na huduma za msingi za kibinadamu zinapatikana.

Mmoja wa wakazi wa kambi hizo mpya mjini Mogadishu ni Bi. Adimo Mohammed ambaye anasema maisha katika kambi za awali yalikuwa dhalili na wanawake na watoto wa kike walikumbwa na ukatili wa kingono, lakini katika makazi mapya hali ni shwari.

(SAUTI (Somali), Adimo Mohamed, IDP)

Kwa sasa makazi hayo mapya yanahifadhi familia Elfu tano lakini  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa katika misaada ya kibinadamu Kilian Kleinschmidt anasema familia zaidi zitahamishiwa makazi mapya.

(SAUTI Kilian Kleinschmidt, )

Huduma za misaada ya kibinadamu nchini Somalia zimeripotiwa kuimarika ambapo idadi ya watu wanaohitaji misaada ya dharura katika miezi sita iliyopita imepungua kwa asilimia Hamsini.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031