Viongozi wa Afrika watakiwa kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira

Kusikiliza /

Makao Makuu ya UNEP, Nairobi Kenya

Viongozi wa mataifa ya Afrika wametakiwa kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira katika kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazoshuhudiwa kwa sasa zikiwemo kuchafuka kwa hewa na athari za kemikali kwa afya na mazingira kwa mujibu wa ripoti ya mazingira iliyotolewa hii leo la Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani, unaoelekea kukamilika mjini Nairobi , inajulikana kama African Environment Outlook na inaangazia masuala kadha yakiwemo uhusiano uliopo kati ya afya na mazingira ikisema kuwa athari za mazingiaira huwa zinachangia asilia 28 ya mzigo wa magonjwa kwenye bara la Afrika.Ripoti hiyo pia imezungumzia suala la ukosefu wa mikakati ya kukabilina na mabadiliko ya hali ya hewa hasusan ukosefu wa maji na usafi. Terezya Luoga Huvisa ni Waziri wa mazingira chini Tanzania.

 

(SAUTI YA HUVISA

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930