Vifo vitokanavyo na Hepatitis E vyaongezeka Sudan Kusini:UNHCR

Kusikiliza /

Wakimbizi Sudan Kusini wakisaka maji

Shirika la kudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi huko Sudan Kusini waliokufa kutokana na ugonjwa wa ini aina ya E, au Hepatitis E imeongezeka na kufikia zaidi ya 111 tangu mwezi Julai mwaka jana.

UNHCR imesema idadi ya walioambukizwa nayo imefikia zaidi ya Elfu sita na takwimu hizo zilikusanywa na shirika la afya duniani WHO na serikali ya Sudan Kusini.

Idadi kubwa ya vifo na wagonjwa ni katika kambi ya Yusuf Batil kwenye jimbo la Upper Nile inayohifadhi wakimbizi zaidi ya Elfu 37.

Wakimbizi wengi kwenye kambi hiyo wanaambukizwa ugonjwa huo wa homa ya ini aina ya E, kutokana na uhaba wa vyoo na kutumia maji yasiyo safi na salama ambapo UNHCR inaamini kuwa ongezeko la wagonjwa linatokana na kumiminika kwa wakimbizi kutoka jimbo la Blue Nile.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA Adrian)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930