Utulivu wa eneo la Afrika Magharibi watikiswa na wasafirishaji haramu: UM

Jalada la ripoti hiyo ya UNODC

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa usafirishaji wa madawa ya kulevya aina ya Cocaine, usafirishaji haramu wa binadamu na madawa bandia yanahatarisha utulivu wa nchi za Afrika Magharibi.

Ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa linalodhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC imesema kuwa mambo hayo yanayoendeshwa na magenge ya uhalifu ya nchi mbali mbali yenye ushirikiano wa kisiri, yanaathiri shughuli na mipango halali ya nchi husika.

Mathalani ripoti hiyo imesema faida itokanayo na biashara ya Cocaine pekee bado ni kubwa kuliko bajeti za usalama wa Taifa kwa nchi kadhaa za Afrika Magharibi, hali inayosababisha ugumu wa usimamizi wa sheria.

Kwa mujibu wa UNODC, takribani tani 50 za Cocaine kutoka nchi za Andean zilizo Amerika ya Kusini husafirishwa kwenda Ulaya kila mwaka kupitia Afrika Magharibi zikiwa na thamani ya mtaani ya dola Bilioni Mbili

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2016
T N T K J M P
« sep    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31