Ushirikishaji jamii dhidi ya ukeketaji ndio siri ya mafanikio: Babatounde

Kusikiliza /

Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na mangariba wa jamii ya Bondo nchini Sierra Leone

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA, Dkt. Babatunde Osotimehin amesema siri ya mafanikio ya vita dhidi ya ukeketaji wanawake na watoto wa kike ni ushirikishaji wa dhati wa jamii husika.

Dkt. Osotimehin ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa UNFPA imekuwa inahakikisha kuwa inafanya hivyo ili hata baada ya kutoa ujumbe kwa jamii, ujumbe huo unakuwa endelevu na unaendelea kutekelezwa siku hadi siku.

(SAUTI BABATOUNDE)

"Kwa kila hatua tunayochukua kwenye jamii ile tunayoanza nayo ni mazungumzo na jamii, halafu tunashirikisha wapatanishi ambao wanaheshimika kwenye jamii, tunawaeleza suala lenyewe ili baada ya kuacha ujumbe unakuwa endelevu. Hii ni kwa sababu unaweza kwenda na kuzungumza na kujaribu kufanya kazi na wataalamu wa afya lakini hilo halitoshi. Jambo muhimu ni kwamba tunaelewa mfumo wa uongozi  wa jamii, watu muhimu katika jamii, tunazungumza nao ili  waelewe na wakubali jambo  hilo na ndio maana tumeweza kufika hapa tulipo leo."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031