Usalama na haki za binadamu bado changamoto Sudan Kusini: UM

Kusikiliza /

Hilde Johnson, Mwakilishi wa Katibu mkuu wa UM Sudan Kusini

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan Kusini, UNMISS Hilde Johnson amesema mwaka mmoja na nusu wa taifa la nchi hiyo umekumbwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa, Bi. Johnson ambaye pia ni mwakilishi maalum wa katibu mkuu huko Sudan Kusini, ametolea mfano kuwa jeshi la polisi la nchi hiyo licha ya kwamba ni kubwa lakini bado halina uwezo wa kudhibiti usalama wa raia.

(SAUTI YA HILDE-Police)

Halikadhalika Mkuu huyo wa UNMISS amesema visa ukiukwaji wa haki za binadamu  na unyanyasaji ikiwemo wa waandishi wa habari na wanaharakati vimeongezeka na wamepinga vikali na tayari Rais wa Sudan Kusini amesema hilo si sahihi na wahusika wajirekebishe.

(SAUTI YA HILDE-Rights)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031