Waliotumia madawa ya kulevya na harakati za kujikomboa

Kusikiliza /

Madawa ya kulevya yameendelea kuwa tishio siyo tu kwa uchumi wa nchi kwa kuwa vijana wanatumbukia katika lindi hilo na kushindwa kufanya kazi, bali pia kijamii kwa kuwa waathirika wa madawa hayo wanashindwa kufanya kazi na hata kuleta mizozo ya kijamii ndani ya familia na jamii zao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kupambana na dawa za kulevya na vitendo vya uhalifu UNODC imekuwa ikiongoza harakati mbali mbali ikiwemo kusaidia wale wanaotumia madawa ya kulevya kurejea katika maisha ya kawaida.

Tanzania ambayo ni moja ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa imeitikia wito wa kupambana na madawa hayo ambapo serikali kwa kushirikiana na mashirika ya kiraia inaendesha kampeni yenye shabaha ya kuwafikia watumiaji wa madawa hayo. Moja ya kampeni hizo ni ile ya kuanzisha vituo maalumu vinavyotumika kutoa ushauri nasaha kwa vijana walioathirika na matumizi ya madawa hayo. Mwenzetu George Njogopa ndio amefuatilia harakati hizo na fuatana naye basi katika makala hii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031