UNICEF yaelezea kushtushwa na mauaji ya watoto 70 kwa makombora Aleppo

Kusikiliza /

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watoto 70 katika shambulizi la makombora katika maeneo ya makazi mjini Aleppo, Syria, mnamo tarehe 18 na 22 Februari.

Katika taairfa yake, Mkurugenzi wa UNICEF katika katika kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Maria Calivis, amesema raia waliuawa katika mashambulizi manne tofauti ya makombora, ambayo yalirushwa mitaa ya Jabal Badro, Tareeq Al-Bab, Ard Al-Hamra, na Tel Rifa't, nje kidogo ya Aleppo.

UNICEF imelaani mashambulizi hayo vikali, na kutoa wito kwa pande zote katika mzozo kuhakikisha kuwa raia, hususan watoto, wanalindwa nyakati zote kutokana na mzozo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031