UNHCR kusambaza ATM kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

 

Wakimbizi wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limepanga kupanua huduma yake ya usambazaji wa misaada ya fedha kwa njia ya mashine zinazojiendesha yaani ATM kwa mamia ya wakimbizi wa Syria walioweka kambi kaskazini mwa Lebanon.

UNHCR imesema kuwa hadi kufikia Marchi mwaka huu inaamini itakuwa imesambaza kadi za atm kwa zaidi ya wakimbizi 30,000.Hatua hii inafuatia kukamilika kwa mpango wake wa majaribio uliofaulu kwa familia 200.

Mradi huo unawalenga zaidi wakimbizi ambao wapo katika hali ngumu ambao watasambaziwa fedha kwa ajili ya kumudu mahitaji yao ya kila siku ikiwemo chakula.

Wakimbizi hao hata hivyo hawajibiki kurejesha fedha hizo ambazo pia zitasaidia mzunguko wa fedha kwenye maeneo yao na y a karibu

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2015
T N T K J M P
« dis    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031